.

.

.

.

Sunday, July 26, 2009

UTABIRI WA SHEIKH YAHYA HUSSEIN


Sheikh Yahya Hussein ameibuka na utabiri wa mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ule unaodai kuwa kuna rais wa nchi moja ya mashariki mwa Afrika atatekwa akiwa kwenye ndege au kupinduliwa.
Sheikh Yahya amewaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo, litatokana na hali ya kupatwa kwa jua kulikotokea juzi nchini China na kwingineko barani Asia.
Ameendelea na kutabiri kuwa pia kutatokea matatizo katika mambo ya ulinzi na usalama kwa viongozi wa nchi mbalimbali za mashariki ya Afrika.
Hata hivyo, hakutaja nchi yoyote ambayo itakumbwa na tukio hilo.
"Pia natabiri baadhi ya wabunge kadhaa kufungwa na wengine kufa ghafla," akasema.
Akaongeza kuwa vilevile, baadhi ya maofisa wa ngazi za juu serikalini watafukuzwa kazi wakiwa nje ya nchi zao kwa kashfa mbalimbali.
Ameendelea kueleza kuwa vyama vya siasa vinavyotawala na vile vya upinzani vitakuwa na mabadiliko makubwa.
Aidha, akasema kuwa Muungano wa Tanzania utaendelea kudumu licha ya watu kulalamikia kasoro kadhaa kila kukicha.

No comments:

Post a Comment