.

.

.

.

Thursday, September 03, 2009

AACHWA KWENYE MATAA

Katika hali isiyo ya kawaida, Bwana Harusi ameachwa solemba kanisani baada ya mwanamke aliyetarajia kufunga naye ndoa, kuingia mitini dakika chache kabla ya kupanda kilingeni kufunga ndoa.
Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi katika kijiji cha Lowa kata ya Nyandekwa Wiayani Kahama baada ya bibi harusi huyo, aitwaye Minza Mathayo, kubadili uamuzi wa kufunga ndoa na kuamua kuingia mitini.
Mmoja wa wana kamati wa kufanikisha ndoa hiyo ambayo ilikuwa ifungwe kwa imani za makanisa ya Kilokole, Bi. Mary Kadonya ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, amesema wakati wakielekea kanisani kwa ajili ya kufungisha ndoa hiyo, bibi harusi alianza kuangua kilio.
Akasema kutokana na hali hiyo baba mdogo wa
Bi. Harusi huyo aitwaye Samweli Golani alimuuliza kwa nini alikuwa akilia wakati siku hiyo ni ya furaha kwake.
Amesema bibi harusi huyo alimweleza baba yake mdogo kuwa hataki kufunga ndoa hiyo kwa sababu Bwana Harusi alikuwa na umri mkubwa kuliko yeye na pia hakuwa tayari kwenda kupima virusi vya Ukimwi.
Diwani huyo amezidi kuiambia Alasiri kuwa baada ya maelezo hayo, baba mdogo wa Bi. Harusi huyo aliridhika na madai ya binti yake na hivyo akaamua kumpakia kwenye gari na kuondoka naye kwenda Kahama Mjini.
Amesema baada ya baba mdogo kutoweka na bibi harusi, Bwana harusi alibakia kanisani akiimba nyimbo za mapambio za kushukuru Mungu kwa yote yaliyomtokea siku hiyo.
Hata hivyo baadhi ya vyombo vya kutetea haki za watoto wilayani hapa vimedai kuwa kitendo cha Bwana harusi kutaka kufunga ndoa na mtoto wa miaka 14 ni makosa kwa mujibu sheria za kujamiiana ni kosa la jinai.
Imedaiwa bwana huyo ana umri wa miaka 44 hivyo akaamua kumpakia kwenye gari na kuondoka naye kwenda Kahama Mjini.
Amesema baada ya baba mdogo kutoweka na bibi harusi, Bwana harusi alibakia kanisani akiimba nyimbo za mapambio za kushukuru Mungu kwa yote yaliyomtokea siku hiyo.
Hata hivyo baadhi ya vyombo vya kutetea haki za watoto wilayani hapa vimedai kuwa kitendo cha Bwana harusi kutaka kufunga ndoa na mtoto wa miaka 14 ni makosa kwa mujibu sheria za kujamiiana ni kosa la jinai.
Imedaiwa bwana huyo ana umri wa miaka 44

No comments:

Post a Comment