Rufaa ya mwanamuziki maarufu, Nguza Viking (pichani kulia) maarufu kwa jina la Babu Seya na wanawe watatu, imeahirishwa hadi Desemba 3 mwaka huu, ili upande wa Jamhuri uweze kupitia nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi.Katika rufani hiyo pia wamo watoto wake ambao ni Papii Nguza, Nguza Mbangu na Francis Nguza ambao wanapinga hukumu waliyohukumiwa kutumikia jela maisha iliyotolewa mwaka 2004 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment