.

.

.

.

Monday, January 04, 2010

WATZ NA WAIVORIAN KUKIPIGA LEO

TIMU ya Taifa 'Taifa Stars', leo jioni inashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza na Ivory Coast 'The Elephants', mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Kikosi cha Ivory Coast kinachojiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika itakayoanza Januari 10, mwaka huu, kilitua nchini mwishoni mwa wiki kikiwa na wachezaji 23, wakiwemo nyota wao wanaokipiga katika klabu mbalimbali za Ulaya.Akizungumzia mechi ya leo, Kocha Mkuu wa Stars, Marcio Maximo, alisema endapo watashinda mechi ya leo, watakuwa wameitangaza vizuri Tanzania, kutokana na dunia nzima kushuhudia mchezo huo."Ni mechi ngumu na ya kihistoria, lakini tunahitaji ushindi ili tuweze kujitangaza kisoka, nawaamini wachezaji wangu na wameahidi kucheza kufa au kupona ili waibuke na ushindi," amesema Maximo.Amesema ni fahari kuona timu yake ikicheza na timu yenye nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa Ulaya, hivyo ataiaga Tanzania kwa kuonesha kandanda safi na kuibuka na ushindi," amesema.Maximo amesema kujiamini kwake kunatokana na wachezaji wake kuwa na uzoefu wa kutosha kwani tayari walicheza na timu kubwa za Afrika zikiwemo Senegal, Ghana na Cameroon na waliweza kuonesha kandanda safi.Naye, Kocha Mkuu wa Ivory Coast, Vahid Halihodzic alisema pamoja na wachezaji wake kuwa na uchovu wa safari, mechi ya leo haihofii sana kwani nguvu zake amezielekeza kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyikia Angola."Ni mechi nzuri na ya kihistoria hasa kwa Tanzania, sina hofu na mchezo wa leo kwani akili yangu yote ipo Angola kwenye michuano hiyo," amesema Halihodzic.

No comments:

Post a Comment