.

.

.

.

Sunday, May 02, 2010

UMISS MKOANI ARUSHA

Kampuni ya Sophy Entertainment ya mjini Arusha imeandaa shindano la Miss Arusha City Center inayotarajia kufanyika May 7 katika ukumbi wa Naura Spring katika jiji hilo.

Akizungumza na Mtaa kwa Mtaa kwa njia ya simu muandaaji wa shindani hilo, Bi. Sophia Urio alisema kuwa shindano hilo linatarajia kuwa na msisimko kwa vile linawashiriki wenye mvuto na wenye muonekano wa ukweli katika uga wa ulimbwende.
Bi. Urio alisema kuwa kwa sasa warembo hao wapatao kumi wapo kambini wakijinoa vilivyo tayari kujiandaa kwa ajili ya mashindano hayo.
Amesema kuwa mataji yanayotarajiwa kushindaniwa na warembo hao yatakuwa ni Mane,ambayo ni kipaji, photogenic, balozi na Miss Arusha City Centre.
“Kiukweli najua mashindano ya mwaka huu yatakuwa na msisimko mkubwa kutokana na maandalizi yake kuwa ni mazuri, Walimu wanaowanoa walimbwende ni watu ambao wanajua wanachokifnya na wamebobea,kwa haili hiyo lazima kutakuwepo na utofauti mkubwa,” alisema Bi. Urio.
Kwa upande wake Rachel Michael ambaye ni mwalimu wa Catwalk alisema kuwa anashukuru sana kuona warembo wanaonyesha kuwa na ushirikiano pamoja na kujituma kwa moyo mmoja katika mazoezi yao,jambo ambalo linampa faraja hata yeye mwalimu wao.
Nae Doreen Mecky ambaye pia ni mwalimu wa kucheza (dance) alisema kuwa warembo wamejifua vya kutosha na hana shaka katika kinyang’anyiro hicho.
Bi. Urio aliongeza kuwa katika shindano hilo litapambwa na msanii Prezoo kutoka nchini Kenya, Hussein Machozi pamoja na kikundi cha ngoma za asili kutoka jijini humo.

No comments:

Post a Comment