TANZANIA ILISHEHEREKEA MIAKA 46 YA MUUNGANO WA NCHI YETU HAPA UINGEREZA MAJUZI KWA IBADA MAALUM ILIYOANDALIWA NA KANISA LA WESTMINISTER ABBEY,LILILOPO WESTMINISTER HAPA LONDON, UINGEREZA.
KANISA HILO LA WESTMINISTER ABBEY,HUANDAA IBADA MAALUM KILA MWAKA KWA NCHI ZILIZO MWANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA (COMMONWEALTH COUNTRIES) KILA MWAKA NCHI HIZO ZINAPOFIKIA SIKU YA UHURU WA MATAIFA YAO.
UBALOZI WA TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA VIONGOZI NA WAWAKIRISHI WA JUMUIYA MBALIMBALI ZA WATANZANIA HAPA NCHINI UINGEREZA, WALISHIRIKI VYEMA KUIWAKIRISHA NCHI KATIKA IBADA HIYO. MISA MAALUM ILIO ANDALIWA NA KANISA HILO MWAKA HUU ILISOMWA NA DADA CAROLINE CHIPETA, MKUU WA UTAWALA UBALOZI WA TANZANIA - HAPA NCHINI UINGEREZA.
No comments:
Post a Comment