.

.

.

.

Saturday, August 07, 2010

KUMBUKUMBU YA BABA YETU MPENDWA


Ni mwaka Mmoja tangu ututoke Tarehe 7/8/2009 saa moja jioni Mpendwa baba yetu Mzee MADAHA GEORGE MALONGO. Haikuwa rahisi kupokea machungu ya kukukosa wewe kwenye maisha yetu hasa kwa sababu ulikuwa chanzo cha vicheko katika kufurahia maisha yetu, lakini kwa baraka zake muumba, tunaamini uko katika pumziko la milele. Tunakushukuru kwa kutuleta duniani na kutufundisha, upendo, ukarimu, ucheshi, na kumpenda Mungu.

Ingawa hauko nasi kimwili lakini kiroho uko pamoja nasi na utaendelea kuwaka kama NURU katika mioyo yetu, kwakua bado tunayaona matendo yako katika maisha yetu. ASANTE SANA BABA.

Unakumbukwa na MKEO ,WANAO , WAJUKUU NA WADOGO ZAKO pamoja na Wazazi wenzako na familia zao, Majirani zako Dsm na Mwanza na marafiki zako
.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

1 comment:

  1. Tupo pamoja katika kumbukumbu za mpendwa baba yenu. Mungu awape uwezo wa kuyaendeleza yale yoto mazuri yake, na kujenga mji wake daima dumu

    ReplyDelete