.

.

.

.

Monday, August 16, 2010

MISS TANZANIA 2010 WAJIKITA KAMBINI


.
Warembo wakiwa ndani ya basi tayari kwa safari ya kambini.

Warembo waliofanikiwa kuingia Fainali ya Taifa ya Mashindano ya Urembo ya VODACOM MISS TANZANIA 2010, waingia kambini siku ya leo “Jumatatu” tarehe 16 / 08 / 2010 katika hatua ya mwisho ya kinyang’anyiro cha kumsaka mrithi wa MRIAM GERALD ambaye anamaliza muda wake wa kuwa Mrembo wa Taifa.

Wakiwa kambini warembo hawa watakuwa na ratiba mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufanya kazi za kijamii na kutembelea sehemu mbali mbali za vivutio vya kitalii kama ifuatavyo:-

· Tarehe 17 / 08 / 2010 warembo watapewa semina maalumu na viongozi wa kamati ya Miss Tanzania pamoja na kusaini mikataba kati yao na waandaaji.

· Tarehe 19 / 08 / 2010 waandishi wa habari wote watapata nafasi ya kuongea na washiriki na kupata maoni yao na jinsi walivyojiandaa katika kunyakuwa taji la VODACOM MISS TANZANIA 2010

· Mwishoni mwa wiki warembo wote wakiambatana na baadhi ya viongozi wa kamati watasafiri kwenda katika mikoa ya kanda ya kaskazini “KILIMANJARO: na “ARUSHA” kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii ili kuvitangaza na kuwahamasisha watanzania ili wajenge utamaduni wa kutembelea, kuvilinda na kuvithamini vivutio vyetu. Huu ni mpango tunaoshirikiana na taasisi za serikali yaani ,BODI YA UTALII, TANAPA na NGORONGORO CONCERVATION AREA AUTHORITY.

Huu ni mwaka wa pili taasisi yetu “Miss Tanzania” kushirikiana na taasisi za serikali kuhamasisha watanzania kuthamini na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu.

Tunategemea kwenda mbele zaidi kwa kuvitembelea vivutio vya kusini mwa Tanzania, SELOUS, RUAHA NATIONAL PARK, MIKUMI na UDIZUNGWA, katika siku za usoni.

Walimbwende walioingia kambini leo ni:-
Ester Dennis na Gloria Kaale,Shadia Mohammed, Furaha David na Mary Kagali ,Bahati Chando, Salma Mwakalukwa na Consolata Lukosi,
Beatrice Premsingh, Willemi Etami na Pili Issa, Flora Florence, Mary Adam na Angelina Ndege.

Wengine ni Alice Lushiku, Irene Hezron, Amisuu Malick ,Genevive Emmanuel, Anna Daudi na Britney Urassa,Glory Mwanga, Prisca Mkonyi na Jally Murei,Gloria Mosha na Christine Justine,Flora Martin, RachelSindbad, PendoSam Fatma Ibrahim, Buduri Ibrahim na Margareth Godson.
Fainali za mashindano hayo makubwa ya Urembo nchini yanataraji kufanyika Septemba 11 2010 jijini Dar es Salaam
Hashim Lundenga
Mkurugenzi.

1 comment:

  1. very excited about Miss Tz....pass by laprincesasworld.blogspot.com..jis showing some love!!!

    ReplyDelete