.

.

.

.

Tuesday, August 31, 2010

PRECISION AIR YAONGEZA MWALI MPYA


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mohammed Babu akikata utepe kama ishara ya kuzindua ndege mpya ya Precision ART 42- 500 iliyopewa jina la "Bukuoba" yenye uwezo wa kubeba abiria 48 ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba na kurudi Dar es salaam, ndege hiyo iliruka kutoka Dar es salaam kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank, Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk
John Bukuku wa FULLSHANGWE akijiandaa kushuka mara baada ya ndege hiyo kurejea Dar es salaam ikitokea Zanzibar jana.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank na mwisho kushoto ni Lucy Malu Meneja Mkazi Kenya Airways.
Hii ndiyo ndege mpya ya Precision Air ATR 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abilia 48 itakayofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba.
baadhi wa Marubani wa Precisiano Air wakiwa katika uzinduzi huo jana.
Meneja wa Uhusiano wa Kampuni ya SCANAD Barnabas Lugwisha akiwa na mmoja wa waalikwa katika ndege hiyo mpya ilifanya safari kati ya Zanzibar na Dar es salaam jana kwa ajili ya uzinduzi rasmi.

No comments:

Post a Comment