
Urban Pulse Creative leo ilipata fursa ya kuingia kwenye Kipindi Sporah show kinachorushwa hewani na Ben TV hapa UK pamoja na Star Tv Tanzania ili kufanya kampeni ya Urban tour kwa ajili ya kusaidia na kuchangia vita dhidi ya Malaria. Ugonjwa huu unaua mamilioni ya watu wengi duniani kuliko Ukimwi, kitu cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba unaweza kutokomezwa na kuangamizwa milele ikiwa kila mtu akielimika na kuamua kuchukua majukumu ya kuviangamiza vijidudu hivi hatari kwa kuanzia kusafisha na kutunza mazingira bila ya kulaumu wala kunyooshea vidole serikali pekee wala Taasisi zozote.
Urban Pulse Ikishirikiana Na Aset pamoja na Tanzania Community inawaletea Msanii Daimond kutoka Tanzania pamoja na Mish the Fyah Sis Kutoka urban Pulse ili kuwapa burudani murwa. Baadhi ya mapato yatakayo patikana yatakwenda kuchangia Kampeni ya kupambana na Malaria in Africa. Wote Mnakaribishwa. Tafadhali wahi mapema. Terehe na ukumbi ni kama zifuatavyo:
6th Nov. 2010
CLUB OPUS
Theatre Distric
Savoy Cresent
Milton Keynes MK9 5UP
12th Nov 2010
THE CLUB
179 – 183 London Road
Croydon, London
CRO 2LR
27th Nov 2010
PANAMA BAR
Gas ST
Birmingham
B1 2JT
WOTE MAKARIBISHWA,
Frank Eyembe
URBAN PULSE CREATIVE MEDIA
No comments:
Post a Comment