
.

.

Sunday, February 27, 2011
Saturday, February 26, 2011
BONGO FLEVA YAINYUKA BONGO MUVI 2-0 JIONI HII




Timu ya Bongofleva FC wametoka kifua mbele jioni hii ndani ya uwanja wa Taifa,mara baada ya kuinyuka bila huruma timu ya Bongo Movie Fc goli 2-0 . Timu ya Bongo Movie ambayo ilionekana kuwa na mbwembwe nyingi uwanjani hapo huku wakiongozwa na kamati yao ya Ufundi ikiongozwa na Bi Mwenda,walionekana kukosa raha na kufadhaika mno kwa kipigo hicho,kama vile haitoshi mchezaji Benn Kinyaiya alizidi kuwatia uchungu wachezaji wenzake kwa kukosa penati iliyokuwa ya wazi kabisa.Mechi hii imefanyika jioni ya leo kwa hisani ya kuchangia watu waliopatwa na maafa/waathiriwa na milipuko ya mabomu iliyotokea kambi ya jeshi Gongo la Mboto hivi karibuni jijini Dar.
WASHIRIKI WA TUZO ZA KILI 2011
MSANII WA KIKE BORA WA MUZIKI.
- Lady Jaydee
- Mwasiti
- Linah
- Shaa
- Khadija Kopa
MSANII WA KIUME BORA WA MUZIKI
- 20%
- Ally Kiba
- Barnaba
- Diamond
- AY
- Belle 9
- 20%
- Barnaba
- Ally Kiba
- Banana
- Belle 9
- Diamond
- Lady Jaydee
- Linah
- Mwasiti
- Khadija Kopa
- Shaa
- My Valentine - JAHAZI
- Top In Town - KHADIJA KOPA
- Acheni Kuniandama - ISHA RAMADHANI MASHAUZI
- Langu Rohoni - JAHAZI
- Mama nipe Radhi - ISHA MASHAUZI
- Mama Ntilie - GELLY WA RYMES ft, AT & RAY C
- Sina Raha - SAM WA UKWELI
- Ya nini Malumbano - 20%
- Mkono Mmoja - CHEGE & TEMBA ft, WAHU
- Bado Tunapanda - TIP TOP CONNECTION
- Tamaa Mbaya - 20%
- Shika Ushikapo - MAPACHA WATATU ft MZEE YUSUPH
- Laptop - EXTRA BONGO
- Kauli - TWANGA PEPETA
- Mapenzi hayana kiapo - TWANGA PEPETA
- Pongezi kwa Wanandoa - AKUDO
WIMBO BORA WA R&B
- Wewe ni wangu - BELLE 9
- Nikikupata - Ben Poul
- Hello - HUSSEN MACHOZI ft MAUNDA ZORRO
- Atatamani - LINAH
- Kisiwa cha Malavidavi - Z-Anton
WIMBO BORA WA HIP HOP
- Propaganda - FID Q
- Karibu Tena - JOH MAKINI
- Ukisikia Paah - JCB ft, FID Q & CHIDI BENZ
- Usije Mjini - AY & MWANA FA
- Higher - NICK WA PILI ft JOH MAKINI
- Sauti ya Rasta - RAS RWANDA MAGERE
- Misingi ya Rasta - WORRIORS FROM THE EAST
- Sayuni - JHIKO MAN
- Ujio Mpya - HARDMAD ft, ENIKA
- Reggae Swadakta - BOB LAU MWALUGAJA
- What u Feel Inside - HARDMAD
- Nimefulia - BENJAMIN WA MAMBO JAMBO ft AT
- Action - CPWAA ft DULLY, NGWEAR & MS TRINITY
- Far Away - BIG JAH MAN ft, RICHARD
- My Friend - BENJAMIN
- Kiuno weka Busy - JET MAN
- Ferguson
- Khalid Chokoraa
- Totoo ze Bingwa
- Kitokololo
- Msafiri Diof
- Fid Q
- Joh Makini
- Ngwear
- Chidi Beenz
- Godzilla
- Nitafanya - KIDUMU & JAY DEE
- Kare - P-UNIT
- Songambele - ALPHA ft AY
- Vuvuzela - GOODLIFE
- Kasepiki - BEBE COOL
- 20%
- Barnaba
- Lady Jaydee
- Mrisho Mpoto
- Mzee Yusuph
MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA WA NYIMBO WA MWAKA
- Marco Chali
- Lamar
- Man Water
- Bob Junior
- Pancho Latino
VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA (HOST POPULAR VIDEO OF THE YEAR)
- Mama Ntilie - Gelly wa Rymes ft AT & Ray C
- Oyoyo - Bob Junior
- Ya nini Malumbano - 20%
- Tamaa Mbaya - 20%
- Mbagala - Diamond
- Sam wa Ukweli
- Linah
- Sajna
- Bob Junior
- Top C
- Mama Ntilie - Gelly wa Rhymes ft, AT & Ray C
- Mkono Mmoja - Chege & Temba ft Wahu
- Ahmada - Offside trick ft Bi Kidude
- Ukisikia Paah - JCB ft, Fid Q, Chidi Beenz & Jay Moe
- Dakika Moja - FA & AY ft Hardmad
- Adela - Mrisho Mpoto
- Kariakoo - Mataluma
- Ahmada - Offsidetrick ft, Bi Kidude
- Shangazi - Mpoki ft, Cassim
- Wa Mbele Mbele - Ommy G
- Sina Raha - Sam wa Ukweli
- Ulofa - Top C
- Nabembelezwa - Barnaba
- Bado Robo Saa - Amini
- Bora Nikimbie - Linah
Friday, February 25, 2011
MASHETANI WA DUNIA HII

Mtoto Deus Juma(7)akiwa wadi namba moja katika Hospitali ya Wilaya ya Geita akiuguza majeraha kwenye mikono yake baada ya kuchomwa moto na mama yake mzazi.Picha na David Azaria
----
POLISI wilayani Geita katika mkoa wa Mwanza wamemkamata mwanamke kwa tuhuma za kumuunguza mwanawe kwa maji ya moto mikono yote miwili na kisha kumfungia ndani kwa siku tatu. Mary Dominick anadaiwa kufanya kitendo hicho wiki iliyopita nyumbani kwake katika Mtaa wa Msalala, mjini Geita baada ya kumtuhumu mtoto huyo kuiba Sh 6,000 zilizokuwa ndani ya nyumba. Mtoto huyo, Deus Juma (7) anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kivukoni amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita. Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Abdallah Dihenga alisema walimpokea mtoto huyo juzi akiwa na majeraha mikononi. Akiwa katika wodi namba moja hospitalini hapo chini ya uangalizi wa majirani waliodai ni wanakikundi cha kusaidiana ambacho mama yake ni mwanachama, mtoto huyo alisema siku ya tukio baada ya mama yake kurejea nyumbani akitokea kwenye shughuli zake, alimuita na kuanza kumpiga huku akimtuhumu kuiba fedha licha ya yeye kujitetea. Juma ambaye alikuwa akijieleza huku akilia, alisema, “pamoja na kujitetea kwa muda mrefu lakini mama hakunielewa hata kidogo na kuendelea kuning’ang’aniza kwamba mimi ndiye mwizi niliyemuibia fedha zake,” alisema na kuongeza: “Aliniingiza ndani na kisha kunifunga mikono yote miwili pamoja na miguu kwa mpira wa kufungia mizigo kwenye baiskeli na kuanza kunipiga” . Alidai baada ya kipigo hicho, mama yake hakumfungulia mpira aliokuwa amemfunga miguuni na mikononi hali iliyomlazimu kulala sakafuni kwa siku tatu kabla ya kufunguliwa na kukutwa mikono imevimba.Kwa mujibu wa mtoto huyo, mama yake alipokuta mikono imevimba alichemsha maji ya moto na kumkanda na alipoona uvimbe haupungui, aliamua kuchukua barafu na kumuwekea kwenye mikono. Inaelezwa kwamba jana asubuhi ndipo mtoto huyo alifunguliwa na baada ya kutoka nje, alikimbilia barabarani alipokutana na wasamaria wakampeleka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, Sosthenes Mahushi.Kiongozi huyo wa kitongoji alithibitisha kumpokea mtoto huyo na kisha kumpeleka polisi kabla ya kumfikisha hospitalini hapo. Mtoto huyo alishuhudiwa akiwa na majeraha usoni na kichwani anayodai yalitokana na kupigwa na kipande cha ubao.Vile vile mikono imevimba huku akiwa na vidonda vikubwa katika viganja kiasi cha kushindwa kukunja vidole. Polisi wilayani hapa imethibitisha tukio hilo na kusema mwanamke huyo anashikiliwa na kwamba atafikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika.Wakati huohuo, wanawake waliokutwa hospitalini hapo wakimhudumia mtoto huyo hawakuwa tayari kuzungumza na kuandikwa majina yao gazetini. Pia hapakuwa na ndugu wala jamaa waliopatikana mara moja kuzungumzia undani wa maisha ya mtoto huyo. Mama yake pia hakupatikana kuthibitisha tuhuma kutokana na kushikiliwa na polisi.
Wednesday, February 23, 2011
ALBINO ALIEPOTEA APATIKANA MSITUNI
MTOTO mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Juma Kapela (3) aliyekuwa ameibwa tangu Jumatano iliyopita wilayani Mpanda mkoani Rukwa, amepatikana akiwa hai, lakini akiwa amechanjwa chale mwili mzima na ametelekezwa msituni. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay, jana alithibitisha kupatikana kwa mtoto huyo na kumpokea ofisini kwake, lakini akiwa amechanjwa chale mwili mzima, kutokana na kile kinachoaminika kuwa ni imani za kishirikina na jitihada za kumdhuru kushindikana. Njoolay alisema alimpokea Juma na dada yake ambaye pia ni albino, Wande Kapela (5), ambao walikuwa wamefuatana na bibi yao ambaye pia ni mlezi wao, Maria Elias (60) na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Naomi Nnko. Juma na dada yake, Wande, wamekuwa wakilelewa na bibi yao kijijini Itunya kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika wilayani Mpanda, na Juma aliliripotiwa kuibwa Jumatano iliyopita na mtu asiyefahamika kwa kile kinachodaiwa ni imani za kishirikina. Mkuu wa Mkoa alisema awali mkoa ulipendekeza kuwa watoto hao wapelekwe kuishi kwenye Shule ya Msingi ya Malangali mjini hapa pamoja na wenzao ambao ni albino, lakini baada ya kubaini kuwa bado ni wadogo haikufanyika hivyo lakini sasa wamekubaliwa na wataishi kwenye nyumba ya watoto yatima mjini hapa ya Mt Martin de Pores iliyopo Katandala. “Hii ni faraja kubwa, hata Waziri Mkuu Pinda nilipomfahamisha kuhusu kupatikana kwa Juma akiwa hai, alisema tu ‘Mungu ni Mkubwa’. Nimekuwa nikimjulisha kuibwa kwa mtoto huyu tangu Jumatano iliyopita. Pia nimeendelea kufanya hivyo hadi alipopatikana akiwa hai juzi, na leo muda mfupi ujao nitamtaarifu kuwa watoto hawa sasa wataishi na kutunzwa kwenye nyumba hiyo ya watoto yatima,” alisema Njoolay. Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa, kupatikana kwa Juma kunatokana na msako mkali uliofanywa siku nne mfululizo ukijumuisha Jeshi la Polisi , Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wananchi wa maeneo ya vijiji vilivyopo si tu mwambao wa Ziwa Tanganyika bali pia wilayani Mbozi, Mbeya. Akizungumza kwa Kiswahili kidogo huku akichanganya na Kisukuma, bibi wa watoto hao, Maria, alidai kuwa amekuwa akiishi na kuwatunza watoto hao tangu miaka miwili baada ya baba mzazi wa watoto hao aitwaye Kwangulija Kapela kumtelekeza mama wa watoto hao na kwenda kuishi Urambo, Tabora. Alisema baba huyo ambaye ni mwanawe, alimtelekeza mkewe, Mbaru Busagija, akimtuhumu kumzalia mfululizo watoto albino ambapo alidai kuwa uzazi wa watoto hao umetia nuksi familia yao. Mama yao huyo ameolewa na anaishi pia Urambo . Akielezea mkasa huo, bibi alisema siku ya tukio, Juma alikuwa na dada yake Wande karibu na nyumba yao wakati yeye amekwenda kutafuta mboga ndipo alipotokea mtu wasiyemfahamu na kuwafukuza na kumkamata Juma na kutoweka naye. “Nilipojulishwa kuibwa kwa mjukuu wangu nililia sana ndipo majirani walipokuja na kwenda kutoa taarifa kwa viongozi wa kijiji ambao waliitaarifu Polisi na msako ukaanza,” alisema bibi huyo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Isuto Mantage, alisema hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo na kwamba msako wa kumtafuta mtuhumiwa unaendelea. |
Tuesday, February 22, 2011
MUAMMAR GADDAFI

To the best of my knowledge, Gaddafi is the only world leader to have female bodyguards. All these girls have black belts in karate. They always carry weapons - a submachine gun, five clips of ammunition, a pistol, a revolver and a knife - even in conference rooms. In an assassination attempt on Gaddafi, one of the girls, Aisha, eventually gave her life as she shielded the leader.


Africa's undisputed newly crowned longest-serving ruler,Muammar Gaddafi, who has been in power for 42yrs.
Col Gaddafi led a coup by young army officers in September 1969, then set about establishing his own political system, as laid out in his Green Book; and he's been there ever since.
In 2008 he was named "king of kings" by a meeting of Africa's traditional rulers.
Col Gaddafi led a coup by young army officers in September 1969, then set about establishing his own political system, as laid out in his Green Book; and he's been there ever since.
In 2008 he was named "king of kings" by a meeting of Africa's traditional rulers.
NI MASIKITIKO MAKUBWA .............
![]() |
Jacob Nyajiego (mwenye suti nyeusi) akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyohifadhi miili ya marehemu mke wake, Rozi Nyajiego (34) na watoto wake wawili, Clementina Nyajiego (4) na Stella Nyajiego (miezi 3) waliokufa kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba wakati wa milipuko ya mabomu. Ibada ya kuwaaga ilifanyika nyumbani kwake Mzambarauni, Gongo la Mboto Dar es Salaam. Miili ya marehemu hao ilisafirishwa kwenda Rorya, mkoani Mara kwa maziko. (Picha na Fadhili Akida) |
Sunday, February 20, 2011
HARAMBEE YA " SAIDIA GONGO LA MBOTO " UINGEREZA
Ndugu zetu na marafiki zetu wapenzi kama mnavyo jua wiki hii kuna janga kubwa sana limetokea huko nyumbani Tanzania na maisha ya watu wengi sana yako mashakani.
Watu hawana makazi, watoto wamepotea, wengine wako mahospitalini na hali ya kiuchumi pia ni utata.
Nimefikiria na wenzangu tukaona tuanzishe kitu kinaitwa "SAIDIA GONGO LA MBOTO".
Kwa wale marafiki zetu mliopo UK au popote pale duniani na mtapenda kuchangia tumeona ni bora tukachangia chochote tulicho nacho and then tuwakilishe Ubalozini na majina ya wale wote tuliojitolea chochote ili ubalozi utusaidie kuwakilisha mchango wetu na kutupatia report ni wapi huo msaada umekwenda na kama ni pesa zimefanya kitu gani kwa ajili ya watu hao.
Haijalishi ni kiasi gani cha pesa au kitu gani utatoa, utoe tu kutokana na uwezo ulio nao and 'it will still make a difference to the people out there'. Msaada unahitajika haraka iwezekanavyo na Ukihitaji receipt pia utapata.
KWA WAKAZI WA LONDON NA MIJI YA KARIBU AU KAMA UTA WEZA KUFIKA TUTAKUWA:
AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT
81 BROAD LANE
SEVEN SISTERS
LONDON
NW15 4DW
SIKU: JUMAPILI
TAREHE 27 FEB 2011
MUDA: 3PM - LATE
KWA WAKAZI WA READING NA MIJI YA KARIBU AU KAMA UTA WEZA KUFIKA TUTAKUWA:
VINCENT RESTAURANT
288-290
OXFORD ROAD
READING
SIKU: JUMAMOSI 26 FEBRUARY 2011
MUDA: 3PM - LATE
TAFADHALI LETA CHOCHOTE ULICHO NACHO ILI TUWEZE KUWASAIDIA HAWA NDUGU ZETU WALIO PATWA NA MAAFA HUKO NYUMBANI TANZANIA
KWA WAKAZI WA MIJI MINGINE AMBAO MTASHINDWA KUFIKA LONDON TUNAPANGA UTARATIBU WA JINISI GANI TUNAWEZA KUFIKA KATIKA MIJI YENU KUKUSANYA HIYO MISAADA. TUTAWAJULISHA MARA MIPANGO HII ITAKAPO KAMILIKA.
KAMA WEWE SI MWENYEJI WA UINGEREZA KUMBUKA KWAMBA HII KITU MTU YOYOYTE DUNIANI ANAWEZA KUCONTRIBUTE KWA UWEZO WAKE SO KAMA UNA CHOCHOTE UNAWEZA PIA UKAWEKA KWENYE ACCOUNT IFUATAYO NA TUNAOMBA UANDIKE JINA LAKO AS A REFERENCE ILI TUJUE PESA IMETOKA KWA NANI AND CAN BE ACCOUNTED FOR!!
BANK: BARCLAYS
NAME: MISS SHILLA GABRIEL FRISCH
ACCOUNT NUMBER: 40974382
SORT CODE: 202941
FOR MORE INFORMATION YOU CAN REACH US ON +447527190239 ,
+447404332910 ,
+447876126862 ,
NINGEPENDA MABLOGGER WOTE TUSHIRIKIANE KUHUSU HILI SWALI NA WADAU WETU NYINYI NDIO NGUZO KUBWA ZAIDI ILI HICHI KITU KIWEZE KUFANIKIWA.,AHSANTENI SANA NA MBARIKIWE!!
Watu hawana makazi, watoto wamepotea, wengine wako mahospitalini na hali ya kiuchumi pia ni utata.
Nimefikiria na wenzangu tukaona tuanzishe kitu kinaitwa "SAIDIA GONGO LA MBOTO".
Kwa wale marafiki zetu mliopo UK au popote pale duniani na mtapenda kuchangia tumeona ni bora tukachangia chochote tulicho nacho and then tuwakilishe Ubalozini na majina ya wale wote tuliojitolea chochote ili ubalozi utusaidie kuwakilisha mchango wetu na kutupatia report ni wapi huo msaada umekwenda na kama ni pesa zimefanya kitu gani kwa ajili ya watu hao.
Haijalishi ni kiasi gani cha pesa au kitu gani utatoa, utoe tu kutokana na uwezo ulio nao and 'it will still make a difference to the people out there'. Msaada unahitajika haraka iwezekanavyo na Ukihitaji receipt pia utapata.
KWA WAKAZI WA LONDON NA MIJI YA KARIBU AU KAMA UTA WEZA KUFIKA TUTAKUWA:
AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT
81 BROAD LANE
SEVEN SISTERS
LONDON
NW15 4DW
SIKU: JUMAPILI
TAREHE 27 FEB 2011
MUDA: 3PM - LATE
KWA WAKAZI WA READING NA MIJI YA KARIBU AU KAMA UTA WEZA KUFIKA TUTAKUWA:
VINCENT RESTAURANT
288-290
OXFORD ROAD
READING
SIKU: JUMAMOSI 26 FEBRUARY 2011
MUDA: 3PM - LATE
TAFADHALI LETA CHOCHOTE ULICHO NACHO ILI TUWEZE KUWASAIDIA HAWA NDUGU ZETU WALIO PATWA NA MAAFA HUKO NYUMBANI TANZANIA
KWA WAKAZI WA MIJI MINGINE AMBAO MTASHINDWA KUFIKA LONDON TUNAPANGA UTARATIBU WA JINISI GANI TUNAWEZA KUFIKA KATIKA MIJI YENU KUKUSANYA HIYO MISAADA. TUTAWAJULISHA MARA MIPANGO HII ITAKAPO KAMILIKA.
KAMA WEWE SI MWENYEJI WA UINGEREZA KUMBUKA KWAMBA HII KITU MTU YOYOYTE DUNIANI ANAWEZA KUCONTRIBUTE KWA UWEZO WAKE SO KAMA UNA CHOCHOTE UNAWEZA PIA UKAWEKA KWENYE ACCOUNT IFUATAYO NA TUNAOMBA UANDIKE JINA LAKO AS A REFERENCE ILI TUJUE PESA IMETOKA KWA NANI AND CAN BE ACCOUNTED FOR!!
BANK: BARCLAYS
NAME: MISS SHILLA GABRIEL FRISCH
ACCOUNT NUMBER: 40974382
SORT CODE: 202941
FOR MORE INFORMATION YOU CAN REACH US ON +447527190239 ,
+447404332910 ,
+447876126862 ,
NINGEPENDA MABLOGGER WOTE TUSHIRIKIANE KUHUSU HILI SWALI NA WADAU WETU NYINYI NDIO NGUZO KUBWA ZAIDI ILI HICHI KITU KIWEZE KUFANIKIWA.,AHSANTENI SANA NA MBARIKIWE!!
Subscribe to:
Posts (Atom)