.

.

.

.

Saturday, February 26, 2011

BONGO FLEVA YAINYUKA BONGO MUVI 2-0 JIONI HII

SHABIKI AKIPULIZA VUVUZELA
NYOMI LIKIWA LIMESHENI UWANJANI
BONGO FLEVA
BONGO MUVI


Timu ya Bongofleva FC wametoka kifua mbele jioni hii ndani ya uwanja wa Taifa,mara baada ya kuinyuka bila huruma timu ya Bongo Movie Fc goli 2-0 . Timu ya Bongo Movie ambayo ilionekana kuwa na mbwembwe nyingi uwanjani hapo huku wakiongozwa na kamati yao ya Ufundi ikiongozwa na Bi Mwenda,walionekana kukosa raha na kufadhaika mno kwa kipigo hicho,kama vile haitoshi mchezaji Benn Kinyaiya alizidi kuwatia uchungu wachezaji wenzake kwa kukosa penati iliyokuwa ya wazi kabisa.Mechi hii imefanyika jioni ya leo kwa hisani ya kuchangia watu waliopatwa na maafa/waathiriwa na milipuko ya mabomu iliyotokea kambi ya jeshi Gongo la Mboto hivi karibuni jijini Dar.

No comments:

Post a Comment