.

.

.

.

Thursday, November 13, 2008

IRENE UWOYA ANYWA SUMU KUJIUA KISA MAPENZIMrembo huyo alikunywa sumu Jumapili iliyopita, majira ya saa 5. 00 usiku nyumbani kwao Mbezi, jijini Dar es Salaam.Akiongea na waandishi wetu, mmoja kati ya ndugu wa karibu wa mrembo huyo, ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alisema kuwa chanzo cha kunywa sumu ni mambo ya kimapenzi.“Irene alikunywa sumu majira ya saa tano usiku baada ya kupata chakula cha usiku na kwenda kulala,” alisema mtoa habari huyo.Baada ya kunywa sumu hiyo, ambayo haikuweza kufahamika ni ya aina gani, alichukuliwa na ndugu zake na kupelekwa katika Hospitali ya IMTU iliyopo Mbezi, jijini Dar es Salaam na hali yake ilidaiwa kuwa mbaya.Habari zaidi zinasema kuwa Irene alifikia uamuzi wa kunywa sumu kwa nia ya kutaka kujiua baada ya aliyekuwa mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Samwel ‘kumtema’.Imedaiwa kuwa Samwel alimtema Irene baada ya kumtuhumu kuwa na uhusiano usiofaa na rafiki yake aliyetajwa kwa jina la Adam.Mtoa habari wetu alisema kuwa kuzoeana kwa Adam na Irene kulikuja baada ya mrembo huyo kupewa lifti ya gari na kijana huyo (rafiki wa mpenzi wake) kutoka Arusha kwenda Dar es Salaam.Iidaiwa pia kuwa akiwa Dar, mrembo huyo alikuwa akijirusha na Adam katika viwanja mbalimbali vya starehe, taarifa ambazo zilimfikia Samwel na kumtibua.Kufuatia hali hiyo, Samwel aliamua kumwacha Irene, huku akimtuhumu kwa uhuni na kutokuwa mwaminifu kwake.“Kwakuwa alimpenda sana mwanaume huyo, alimpomwagwa aliamua kuchukua jukumu la kujiua,” alisema mtoa habari wetu.Habari zaidi zinasema kuwa pamoja na kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Adam, pia imedaiwa kuwa kitendo cha kucheza filamu ya uroda kimemkasirisha mno Samwel.Hivi karibuni Irene alicheza filamu inayokwenda kwa jina la ‘Oprah’ wakiwemo Steven Kanumba, ‘Kanumba’ na Vincent Kigosi ‘Ray’.Katika filamu hiyo, Irene aliyecheza kama mke wa Ray alionekana akifanya ‘malavidavi ya kufa mtu’ na Kanumba ikiwa ni pamoja na kuliwa denda ‘laivu’ na mambo mengine yanayoendana na hayo.Waandishi wetu walimpigia simu Irene ambapo ilipokelewa na mdogo wake aliyejulikana kwa jina la Lilian ambaye alidai kuwa dada yake yuko Hospital ya IMTU.Waandishi wetu walikwenda katika Hospitali hiyo na kufanikiwa kuonana na dada yake Uwoya na Lilian wakiwa katika viti vya wagonjwa ambapo waliwaambia wanahabari wetu kuwa hawaruhusiwi kuonana na Irene.Hata hivyo, dada huyo alikataa kuongea chochote juu ya sababu za kutaka kujiua kwa Irene.“Tulipomaliza kula chakula cha usiku tukaagana na kwenda kulala, usiku tulimsikia akipiga kelele, ilikuwa kama saa sita usiku, tulipofungua mlango tukakuta ameshakunywa sumu, ndipo tukamkimbiza Hospital, akatapishwa hadi hivi sasa hali yake si nzuri,” alisema dada’ke Irene.
Source: Risasi Mchanganyiko

9 comments:

 1. Hilo siyo jibu ya kuachwa na mchumba unayependa kwa dhati

  ReplyDelete
 2. Haina haja kujiuwa kisa mapenzi, kwa kuwa Mungu anaweza kukufuta machozi na kukupa mwingine mchumba kwa kuwa yeye si maskini. Mke mwema ao Mme hutoka kwa Bwana

  ReplyDelete
 3. Mrembo na mtu maarufu kama huyo ni aibu kubwa katika jamii kwa sababu anaweza kustopisha shuhuli zake kwa swala la kijinga kama hilo.Infact anamepewa vitu vingi katika maisha yake.Mungu amesema kuwa hawezi kukupa kila kitu .

  ReplyDelete
 4. kujiua sio Kumaliza tatizo ,la muhimu zaidi irine angechukua uamuzi wa kumuelewesha na sijui kama samweli anamapenzi ya dhati asingemuelewa.,pole sana irine kwa kutendwa yote ni sehemu ya maisha ,ucjali mungu atakupatia riziki yako .hila la muhimu zaidi kulitunza penzi lenu kwa kuwa mwaminifu na mkweli .

  ReplyDelete
 5. Mmezidi kuigiza filamu ambazo haziendani na utamaduni wetu, Samweli akiwa kama mwanaume hawezi kuvumilia ujinga kama huo. Kama unataka kujiuwa kweli nenda polini ukanywe hiyo sumu uwone kama htokufa siyo kuuza magazeti.

  ReplyDelete
 6. kiukweli hapo IRINE hajafanya kitu kizuri kwa kweli mana kwanza ametenda dhambi ya mauti kwa hatua hiyo na vilevile kama imeshatokea hamna maelewano baina yake na mumewe ilibidi wayamalize lakini c kutaka kujiua,kwahiyo km angejiua ndo angepata muafaka gani wakati yeye tumeshampoteza......SIO ISHU IRENE ULIVYOFANYA

  ReplyDelete
 7. Huna akili kabisa na Mungu atakuadhibu kwa kitendo ambacho ulitaka kukufanya.Wanaume wapo wengi na unaweza kumpata ambae akawa anakupa furaha kuliko ambae ulitaka kujiua kwa ajili yake.Unachotakiwa umwombe Mungu na sio kujiua.

  ReplyDelete