.

.

.

.

Friday, April 15, 2011

SBL YADHAMINI TUZO ZA TASWA 2011KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL), imetangaza kudhamini Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2010 kwa sh. Milioni 80 zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)..
Tamko la udhamini huo, lilitolewa na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Serengeti, Teddy Mapunda wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam, ambapo fedha hizo zitatumika kwenye masuala mbalimbali.
Mapunda alisema SBL imekuwa jirani na TASWA na ina matumaini makubwa kwamba tuzo za mwaka huu zitakuwa bora zaidi, ambapo zitafanyika hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam Mei 6 mwaka huu.
Naye Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto aliishukuru SBL kukubali kudhamini tuzo hizo na kwamba chama chake kinaendelea kujipanga kuhakikisha tuzo yenyewe inafanikiwa. “Naamini udhamini huu ambao ni wa kwanza mkubwa na wa aina yake katika historia ya tuzo za TASWA, utaleta yale mabadiliko ya kweli ambayo TASWA iliahidi kuhusiana na tuzo hizi. “Niliahidi siku nachaguliwa Agosti 15 mwaka jana kwamba kwa kushirikiana na wenzangu kuna mambo mbalimbali tutaboresha ikiwemo tuzo, ambazo licha ya kuwa ni jambo kubwa lakini ufanyikaje wake haukuwa mwafaka sana.
“Ushahidi wa jitihada za kuboresha tuzo ulianza mwezi mmoja uliopita, wakati Kamati ya Utendaji ya TASWA ilipoamua kuunda Kamati Maalum chini ya Mhariri veteran, Masoud Sanani pamoja na wahariri mbalimbali nchini, kamati ambayo hivi sasa inaendelea na mchakato wa kutupatia wanamichezo ambao tutawazawadia hiyo Mei 6, mwaka huu.
“Lakini ushahidi mwingine ni leo hii, siku ya kihistoria ya kutangaza udhamini wetu, nawashukuru sana SBL na wameonesha kweli wao ni marafiki wa waandishi wa habari na pia ni marafiki wa wanamichezo wa Tanzania,” alisema Pinto.
Alisema tuzo za mwaka huu wamepanga kutumia sh. Milioni 160 na kuwa Serengeti ndiyo mdhamini mkuu, ambapo Movenpick Hotel na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) watakuwa wadhamini washiriki na kwamba wadhamini wengine wanaendelea kutafutwa. Naye Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando alisema tuzo za mwaka huu watazawadia wanamichezo bora kwa kila mchezo na kwamba tayari mchakato wa jambo hilo unaendelea. Wanamichezo Bora kwa miaka ya hivi karibuni na miaka yao kwenye mabano ni wanariadha Samson Ramadhani (2006),

No comments:

Post a Comment