.

.

.

.

Thursday, July 21, 2011

CHAKA KHAN ATEMBELEA MJENGONI (CLOUDSFM)

Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimkalibisha mgeni wake,Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Marekani,Chaka Khan aliyewasili leo mchana kwenye viunga vya ofisi hizo.Mwanamuziki huyo anatarajia kufanya onesho lake Julai 23 ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza,kwa udhamini mkubwa wa Club E.
Joe' akimuongoza mgeni wake,Chaka Khan kwenye ofisi yake leo mchana mara alipowasili ndani ya ofisi za Clouds Media Group,zilizopo Mikocheni jijini Dar.
Mwanamuziki Chaka Khan akigonga na Mtangazaji wa Choice FM,Thandi leo mchana alipokuwa akifanya nae mahojiano mafupi kuhusiana na onyesho lake litakalofanyika ndani ya Ubungo Plaza,July 23 kwa udhamini mkubwa wa Club E.
Mwanamuziki Chaka khan akiwa amepozi na Mtangazaji wa redio ya Choice FM,Thandi mapema leo mchana maara baada ya kufanya nae mahojiano mafupi.
Mwanamuziki Chaka Khan akiacha Chata lake kama ukumbusho wa pekee kwa Kampuni ya Clouds Media Group,huku baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia tukio hilo adhimu.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimuonesha Mwanamuziki Chaka Khan baadhi ya picha za wanamuziki mbalimbali wa Kimarekani na kwingineko waliowahi kufika nchini Tanzania na pia kufanya kazi na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.
Mwanamuziki Chaka Khan akiwa amepozi kwa picha leo mchana na Mkurugenzi wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwa na Mkewe,Mkurugenzi wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd Juhayna Ajmi Kusaga pamoja na mtoto wao Natalia Kusaga .

No comments:

Post a Comment