.

.

.

.

Wednesday, July 20, 2011

TANGAZO LA MSIBA

Ndugu Malumbo S Malumbo ni mwenzetu anaeishi hapa ujerumani, Anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Bw. Hamza S Malumbo kilichotokea Ghafla siku ya jumapili huko Dar es salaam na mazishi yamefanyika katika makaburi ya kisutu siku ya jumatatu.

Kama ilivyo ada kwa watanzania kufa na kuzikana kwetu ni moja ya utamaduni wetu. Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) Unapenda kuwatangazia Watanzania wote wanaoishi hapa ujerumani na nje ya Ujerumani. Tumfariji ndugu yetu Malumbo na Familia ya wafiwa. Kwa kumchangia senti kidogo kama Rambirambi kutoka kwa wanachama/watanzania tunaoishi ujerumani na nje ya ujerumani. Ndugu watanzania mwenye 5 10. 15 euro na kuendelea tunaomba mchango wenu wa hali, ili tumfariji mwenzetu asijione yupo peke yake katika majonzi haya makubwa yaliyomfika. Pesa zitakazopatikana zitakabidhiwa kwa Familia ya Malumbo kama mchango wa Mazishi kutoka kwa Umoja wetu.

Tafadhali unaweza kutuma mchango wako moja kwa moja kwa Bw. Malumbo S Malumbo katika account Namba ifuatayo

Malumbo Salim Malumbo

Acc Nr. 7926977820

Blz. 310 108 33

Santander Consumer Bank

Nitamuomba Bw. Malumbo Kuratibu zoezi hilo kwa kukabidhi majina ya waliochanga kwa kamati ya umoja wa watanzania Ujerumani (UTU) kupitia e mail yetu ya kamati mara baada ya zoezi hili kukamilika, ili kuweka kumbukumbu. Kamati pia itamtumia kila mtanzania orodha ya waliochangia.

Huu ndio Utanzania Halisi wakati wa shida tusaidiane na wakati wa Raha pia tufurahi pamoja.

Umoja wa watanzania Ujerumani umesikitishwa sana na habari hizi za majonzi na unajumuika na Familia ya Malumbo katika kipindi chote cha maombolezi.

Tunamuomba Mwenyezi mungu aiweke roho ya Ndugu yetu Hamza S Malumbo Mahala Pema Peponi

AMIN

Kny

Kamati

Mfundo Peter Mfundo

No comments:

Post a Comment