Haya ni moja ya mavazi yaliowahi kuvaliwa na wasichana warembo katika miaka ya 1960, mavazi haya ni miongoni mwa mavazi yaliyotia fora katika onyesho la mavazi la Redds Night of Fashion linalofanyika jana usiku kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, lengo la onyesho hilo ni kuwapa ubunifu na kuzindua vipaji mbalimbali vya warembo hao katika jumba la Vodacom House ili kuibua vipaji vyao vilivyojificha. Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndiyo wadhamini wakuu wa mashindano ya Miss Tanzania kwa muda mrefu sasa.
Mmoja wa warembo akipita jukwaani na vazi lililowahi kuvaliwa katika miaka ya 1960 na wasichana warembo wa miaka hiyo.
Warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakicheza ngoma ya Lizombe katika onyesho la Redds Night of Fashion katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Mdau huyu naye alikukwepo kama unavyomuona akiwa amekula pozi matata.Warembo hawa wakionyesha mbwembwe za kupiga picha jukwaani.
Mapacha watatu katika mambo ya Libeneke kutoka kulia ni Othman wa Mtaa kwa Mtaa, Issa Michuzi wa Michuziblog na Ahmed Michuzi mzee wa jiachie.
KWA HISANI YA FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment