.

.

.

.

Wednesday, October 12, 2011

ANKAL ISSA MICHUZI ( Mzee Wa Libeneke) KATIKA MIZUNGUKO YA STAREHE JUMAMOSI ILIOPITA


Safari ya wikiendi ya Ankal ilianzia Nyumbani Lounge ambako siku hizi kila Jummosi linaangushwa debe la Old Skul na DJ Peter Moe na wenzake. Kwa kweli hawa jamaa kwa kuchanganya za kale na za leo ni balaa
Nyumbani Lounge pamoja na debe la maana pia wanamuziki huoneshwa moja kwa moja kwenye boti kubwa lililomo ukumbini hapo
Ankal na wadau pamoja na mwenyeji wao Nyumbani Lounge, Gadna G Habash (wa pili shoto)
Baada ya Nyumbani Lounge kituo cha pili kikawa Millenium Towers ambako nako pana debe la kufa mtu chini ya DJ Bonny Luv na Nduguze. Juu Ankal akiwa na wadau hapo Mzalendo Pub
Mdau anayarudi huku DJ MacKay akiskrachi na DJ Bonny Luv akirepui Mzalendo Pub
Ankal anakula konozzzz na Ma-DJ wakongwe. Shoto ni DJ Paul MacGhee, mwenye Bluu ni DJ Mr A akifuatiwa na DJ ELiud Pemba. Aliye kazini ni DJ Mackay
Mzalendo Pub hapatoshagi siku za Jumamolsi
Baada ya Mzalendo Pub Ankal alisogea jirani Kijiji Cha Makumbusho na kukutana na bosi wa Mabibo Kaka Jerome (shoto) na Rais wa FM Academia Prezidaa Nyoshi el Saadat kwenye mambo ya Ngwasuma ya kila Jumamosi mahali hapo

Mwimbaji mkongwe wa FM Academia, Comrade Jesus, akiongoza safu ya mashambulizi ya wana Ngwasuma
Wanenguaji wa FM Academia wakila Ngwasuma la nguvu
Hapo Ngwasuma Ankal alikutana pia na mastaa wa Filamu na wadau wengine
Wadau wakiingia Ngwasuma
Baada ya kuondoka Kijitonyama Ankal alitia timu Salender Bridge Club kwa Wana Njenje ambako alipewa maiki na kurusha mistari miwili mitatu kwa ufanisi kabisa
Msafara ukahamia Mango Garden ambako alikutana na mwimbaji nyota wa Twanga Pepeta Muumini Mwinjuma na mdau
Da' Asha Baraka na mdau wakiwa Mango Garden almaarufu kama Old Trafford ya Twanga Pepeta


PICHA NA HABARI KWA HISANI YA ANKAL

No comments:

Post a Comment