Bendi ya Extra bongo - Next level, wazee wa kizigo Jumamosi iliyopita waliwasha moto wa uhakika ndani ya ukumbi wao wa nyumbani Meeda Sinza, na kuzikonga vilivyo nyoyo za wapenzi wao.
Kumbe nae yumoo!! Hapa Mnenguaji maarufu wa Extra Bongo wazee wa kizigo akiimba ndani ya ukumbi wa Meeda Sinza Jumamosi iliyopita.
Wanenguaji wa kiume nao walizikonga nyoyo za washabiki wao pale walipokata sebene la ukweli, wakiongozwa na Nyamwela mwenye shati jekundu.
Maua ya Extra nayo hayakuwa nyuma yaliwasha moto wa maana mpaka mashabiki wakapagawa.
Shabiki akichezeshwa stail ya Kizigo na Rapa maarufu wa Extra Bongo Fagasoni.
Kwa hisani ya KAPINGAZ
No comments:
Post a Comment