.

.

.

.

Tuesday, October 11, 2011

RAIS ATOA AGIZO TATIZO LA UMEME TANZANIA LISHUGULIKIWE HARAKA

RAIS Jakaya Kikwete amewataka watendaji wake kufanya uamuzi wa haraka bila kigugumizi kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

Amesema wanapaswa kutambua kuwa nchi iko katika hali ya dharura kubwa ya upatikanaji wa nishati ya umeme, na hivyo wafanye uamuzi wa haraka, bila kigugumizi, kukabiliana na hali hiyo kwa manufaa ya wananchi.

“Tuko katika hali ya dharura na mimi sioni hisia za uharaka wa kuchukua uamuzi na hatua nyingine muhimu za kukabiliana na udharura wa upatikanaji wa umeme na nyenzo nyingi za kuzalisha umeme.

“Hatuwezi kuendeleza kuwa na kigugumizi katika kuchukua maamuzi ya kuitoa nchi katika changamoto kubwa hizi za upatikanaji wa nishati,” Rais Kikwete aliwaambia watendaji hao wa Serikali yake wanaohusiana na sekta ya nishati.

“Ubwana mkubwa wa kila mmoja wetu utatambuliwa kutokana na mafanikio ambayo kila mmoja wetu ataonesha katika kuchangia katika kukabiliana na hali hii ya upatikanaji wa nishati,” alisema Rais Kikwete katika kikao cha watendaji hao kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.

Kwa mujibu wa Ikulu, Rais alikuwa anazungumza katika kikao alichokiitisha kuzungumzia ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na upatikanaji wa gesi asilia nchini ili kuzalisha umeme.

Umeme umekuwa katika mgawo nchini tangu Novemba mwaka jana kutokana na ukame ulioathiri kina cha maji katika mabwawa yote ya kuzalisha umeme nchini.

Hali hiyo imeilazimisha nchi kuchukua hatua nyingine za kupatikana kwa umeme wa dharura mbali na hatua ambazo tayari Serikali ya Rais Kikwete ilikuwa imeanza kuchukua kuongeza kasi ya upatikanaji wa umeme kutokana na vyanzo vingine mbali na maji

No comments:

Post a Comment