.

.

.

.

Monday, November 14, 2011

HALI YA UMEME TANZANIA

KAMPUNI ya kuzalisha umeme ya Symbion, imesema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu, itakuwa imeongeza Megawati 60 kwenye Gridi ya Taifa.Hatua hiyo ya Symbioni inatarajiwa kupunguza zaidi makali ya mgawo wa umeme, ambayo kwa sasa unaonekana kupungua ikilinganishwa na awali, kabla ya Serikali kupitisha mpango wa dharura wa nishati ulio na thamani ya Sh 1.2trilioni.

Katika mpango wa dharura uliopitishwa na Bunge Agosti 13 mwaka huu, kampuni ya Symbion walipaswa kuzalisha megawati 205, lakini hadi sasa mitambo ya kampuni hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam, inazalisha Megawati 37 ambazo zimeingizwa katika gridi ya taifa.Kupitia taarifa yake kwa umma iliyoitoa jana Symbion imesema, tayari mitambo ya kuzalisha umeme huo, imewasili nchini kutoka Dubai na inaendelea kufungwa mjini Dodoma.

Msimamizi wa mradi huo Don Brindle jana alimweleza Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na ujumbe uliotembelea eneo inapofungwa mitambo hiyo kuwa, shughuli hiyo inaendelea kwa kasi.“Mitambo iliingia siku chache zilizopita, tunataka kuifunga haraka iwezekanavyo, ili tuweze kulidhibiti tatizo la umeme katika nchi hii,” alisema Brindle.

Brindle alisema, mitambo mingine ya kuzalisha Megawati 145, itaingia nchini mwezi ujao, hali itakayowezesha kampuni hiyo kuzalisha Megawati 242, ingawa katika mkataba wake inatakiwa kuzalisha Megawati 205.Kwa mujibu wa Brindle, mradi huo unaendelea bila kuwepo mkataba (PPA), unaotakiwa kupitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

“Kusema ukweli Symbion imechukua ‘risk’ kubwa sana kibiashara kwa ajili ya kusaidia watu wa Tanzania,” alisema Brindle

No comments:

Post a Comment