.

.

.

.

Sunday, April 08, 2012

ELIZABETH MICHAEL AL-MAARUFU LULU ..........


 Elizabeth Michael au maarufu kama Lulu ambaye kama ilivyokuwa kwa Marehemu Steven Kanumba, naye pia ni muigizaji wa filamu nchini Tanzania(Bongo Movies).
Lulu anatajwa kuwa ndiye mtu ambaye mpaka dakika za mwisho alikuwa na Marehemu.Inaaminika kwamba wawili hao walikuwa wapenzi ingawa waliyafanya kwa siri kwani hivi karibuni wote wawili katika nyakati tofauti kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa kila Jumatatu na East Africa Television, wote walikana kuwa na mahusiano na mtu yeyote.Walisema wapo Single.
Hivi sasa Lulu anashikiliwa na Polisi akiendelea kuhojiwa au kuwasaidia Polisi katika uchunguzi wanaoendelea kuufanya kufuatia kifo cha muigizaji huyo maarufu. Pamoja na kwamba vidole vingi kwa hivi sasa vinamuelekea binti huyu mdogo lakini ambaye mara kwa mara amekuwa akijaza kurasa za mbele za magazeti hususani yale “pendwa”,sisi hapa BC tunadhani ni busara zaidi kama tungeviachia vyombo vya dola(Polisi kwa wakati huu) kufanya uchunguzi wao wa kina kwanza.
Tunaamini kwamba Jeshi la Polisi litaweka hadharani taarifa kamili juu ya uchunguzi wao. 

Tuendelee kumuombea Steven Kanumba apumzike kwa Amani.Amina.


1 comment:

  1. tuiombee nchi yetu na watu wote kwani yaalio andikwa yanatimia

    ReplyDelete