.

.

.

.

Monday, April 09, 2012

KANUMBA KUZIKWA MAKABURI YA KINONDONI KESHO


Ratiba ya awali ambayo imetolewa na Kamati Ya Mazishi ya Muigizaji Steven Kanumba inaonyesha kwamba shughuli za kuuaga mwili wake zitafanyikia katika viwanja vya Leaders jijini Dar-es-salaam kuanzia saa 4 asubuhi na baadae atazikwa katika makaburi ya Kinondoni ambayo hayapo mbali na viwanja hivyo.
Uhakika wa Ratiba hii unafuatia kuwasili kwa mama yake mzazi akitokea Bukoba na yeye kutoa baraka zake kwa mtoto wake kipenzi kupumzishwa hapa hapa jijini Dar-es-salaam.
Mama mzazi wa Steven Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa (katikati aliyeshika tama), akiwa amezungukwa na ndugu,jamaa na waombolezaji wengine mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sinza-Vatican.Picha kwa hisani ya Shamim Mwasha at 8020 Fashions Blog
Steven Kanumba, muigizaji ambaye bila shaka tunaweza kusema ndiye alikuwa maarufu zaidi miongoni mwa waigizaji wa filamu za kitanzania(Bongo Movies) alifariki majuzi alfajiri kuamkia Jumamosi katika mazingira ambayo bado yanatatanisha na bado polisi wanaendelea na uchunguzi ingawa taarifa ya uchunguzi wao wa awali, iliyotolewa na RPC wa Kinondoni,Charles Kenyela, inaonyesha kwamba huenda marehemu amefariki kutokana na matumizi mabaya (alcohol abuse) ya pombe kali aina ya Jack Daniels.
Taarifa hiyo inafuatia mahojiano kati ya Polisi na muigizaji mwingine Elizabeth Michael “Lulu” ambaye inaaminika ndiye alikuwa na Marehemu ambapo awali kabla mauti hayajamkuta palitokea kutoelewana baina yao.Kwa mujibu wa maelezo ya Lulu, Kanumba alikuwa ametumia kinywaji hicho kwa wingi ana wakati wakiendelea na malumbano, alianguka na kujigonga katika ukuta wa chumbani hapo.
Hata hivyo, taarifa ya kitabibu(Post Mortem) kuchunguza chanzo cha kifo chake  bado haijawekwa wazi na  inatarajiwa kufanyika hivi leo(Jumatatu) na ukimalizika basi ndipo taarifa rasmi itatolewa na hivyo kubariki rasmi kuendelea kwa shughuli za mazishi hapo kesho.


 

No comments:

Post a Comment