.

.

.

.

Sunday, June 10, 2012

WAZIRI SAITOTI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya afariki dunia kwenye ajali ya ndege Habari za hivi punde kutoka Nairobi, Kenya zinasema kuwa Helkopta ya polisi iliyokuwa imembeba Waziri wa Usalama wa Taifa, Profesa George Saitoti, naibu wake Orwa Ojode pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini imeanguka na kushika moto. Habari zaidi zinasema maafisa hao wa serikali wamefariki dunia pamoja na walinzi wao na rubani wa helkopta hiyo. Helkopta hiyo iliyokuwa ikielekea katika eneo la Nthiwa nyumbani kwa Bw. Ojode imeanguka katika milima ya Ngon'g nje kidogo ya Nairobi. Helkopta hiyo ilikuwa na watu saba wakati wa ajali. Inafaa kukumbusha hapa kuwa, tarehe kama ya leo miaka minne iliyopita yaani Juni 10 mwaka 2008, helkopta ingine ilianguka na kumuua Waziri wa Barabara, Kipkalya Kones pamoja na Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais Lona Laboso

No comments:

Post a Comment