.

.

.

.

Monday, August 06, 2012

USIKU WA CHEO

Asalaam Alaykum Warahmatu llahi Wabarakatu

LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) NI USIKU AMBAO UNAPATIKANA NDANI YA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI NDANI YA KUMI LA MWISHO MTUME (S.A.W) LILIPOKUWA LIKIINGIA KUMI LA MWISHO ALIKUWA AKIZIDISHA IBADA KWA SANA NA KUWA AMSHA WATU WAKE ( ALHAL BAYTI ) KWA AJILI YA KUFANYA IBADA ZAIDI KATIKA KUMI HILO. LAYLATU QADIR SI MWEZI 27 TU ILA WENGI WA WANACHUONI WAMEJITAHIDI KUWA HIYO NDIO SIKU YA LAYLATUL QADIR SIKU HII INAPATIKANA NDANI YA MWEZI 21 , 23 , 25 , 27 , 29 , NI JUU YETU NDUGU ZANGU KUITAFUTA SIKU HII KWA KUFANYA IBADA KWA WINGI NDANI YA KUMI LA MWISHO ILI M/MUNGU ATUWEZESHE KUIDIRIKI SIKU AMBAYO UBORA WAKE NI ZAIDI YA MIEZI 1000 NA HUSHUKA MALAIKA NDANI YA SIKU HIYO KWA IDHINI YA M/MUNGU SUBHANAHU WATAALAAH . UTUFUKU WA SIKU HII NI UNAPATIKANA KWA MAMBO MAKUU MAWILI KUTEREMKA KWA QUR AN ( MUNGOZO WA MUISLAM) KUSHUKA KWA MALAIKA KWA IDHINI YA MOLA MTUKUFU. NA IBADA YA SIKU HII UBORA WAKE NI ZAIDI YA MIEZI 1000. NI JUU YETU KUHAMASISHANA NAKUKUMBUSHANA KUWA SIKU HII SI SIKU MOJA NA MUHIMU SANA ILI KUPATA KUMUOMBA MUNGU NA KULIOMBEA TAIFA LETU NCHI YETU YA TANZANIA MUNGU KULIPA BARKA. SIKU HII MUNGU AKIKUBARIKI KUIDIRIKI DUA YA KUOMBA NI HII KWA MAELEKEZO YA MAMA AISHA alimuliza Mtume Jee? tukiidiriki LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) tufanye nini ? Mtume akajibu kithrisha kusema NASH-HADU ANLAA ILAAHA ILLA ALLAHU NASTAGHFIRULLAH NAS'ALUKAL JANNATA ILAAHI WANAUDHUBIKA MINA NNAAR ALLAHUMA INNAKA AFUWUN TUHIBUL AFWAA FA'AFUANNAA YAA KARIYMAL AFWU ". Kama alivyosema Mtume MUNGU NDIYE MJUZI WA HII SIKU LAKINI INAPATIKANA NDANI YA KUMI LA MWISHO LA RAMADHANI.

 Ghalib N Monero.
 Al- Azhar University Cairo Misri

No comments:

Post a Comment