.

.

.

.

Monday, September 24, 2012

SERENGETI FIESTA YAFUNIKA IRINGA 
Lina mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva kutoka kundi la THT akicheza na Tausi mmoja wa mashabiki waliojitokeza katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, linalofanyika kwenye uwanja wa Samora Usiku huu mjini Iringa ambapo wasanii mbalimbali wanafanya vitu vyao jukwaani wakiburudisha mashabiki wa mkoa wa Iringa, Lina ameweza kufanya mambo makubwa na kuwaimbisha mashabiki wake ukizingatia kwamba anatoka mkoa huo
 
Meneja Masoko wa kampuni mya Push Mobile Rugambo Rodneyakipiga picha ya pamoja na mmoja wa Ali Mohamed Sanga kazi wa Mshindo Iringa mjini ambaye ni  mshindi wa moja ya  pikipiki
 
Amini akiimba jukwaani katika tamasha hilo
  
Rachel akimwaga mauno jukwaani ametisha kwa ujumla usiku huu mjini Iringa na mashabiki wamemkubali.
usiku huu.
 
Mshindi wa Serengeti Fiesta Super Nyota kutoka mkoani Mbeya anayejulikana kwa jina la Ney Lee akiimba jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa , ambapo wasanii mbalimbali watapanda jukwaani kuburudisha wakazi wa mkoa wa Iringa.
 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva anayekulikana kwa jina la Young Killer akifanya vitu vyake jukwaani  huku
 
Hapa ni Full Kushangweka mwenye kurusha juu ngua haya, mwenye kitambaa mkononi haya mwenye koti haya ilimradi burudani imekolea.
 
Nyomi la mashabiki waliofurika kwenye uwanja wa Samora kwa ajili ya kushuhudia tamasha la Srengeti Fiesta 2012 mjini Iringa

No comments:

Post a Comment