.

.

.

.

Friday, November 09, 2012

MAONYESHO YA UTALII YA DUNIA JIJINI LONDON


 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh . Balozi Khamis Kagasheki akikabidhi zawadi ya Kinyago Leila Ansell kutoka kampuni ya Zara Tours Adventures mara baada ya kuwa miongozi mwa makampuni ya Tanzania yaliyopewa tuzo kwa ajili ya kuuza na kutangaza utalii wa Tanzania katika maeneo mbalimbali duniani hasa Marekani na Ulaya katika Dhifa iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) kwa makampuni yanayoshiriki maonyesho ya Utalii ya Dunia World Travel Market (WTM)katika eneo la Excel jijini London nchini Uingereza , ambapo Balozi Khamis Kagasheki alikuwa mgeni rasmi katika dhifa hiyo akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe.
Katika picha katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Bw. Geofrey Meena
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh . Balozi Khamis Kagasheki akikabidhi tiketi ya ndege kwa Bw. Kamuhanda tiketi iliyotolewa na shirika la ndege la Precision Air nchini Tanzania ambao nao wameshiriki katika maonyesho hayo ya utalii ya WTM nchini Uingereza, Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa shirika hilo Bw. Patrick Ndekana.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh . Balozi Khamis Kagasheki akikabidhi tuzo kwa Bw. John Bukuku Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mtandao wa www.fullshangweblog.comkutokana na mchango wa mtandao huo katika kutangaza utalii nchini Tanzania na duniani kote katikati ni Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) Bw Geofrey Meena.
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh . Balozi Khamis Kagasheki akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Pongo Safari & Tours Bi. Cynthia Ponera katika hafla ya kutambua na kupongeza mchango wa makampuni mbalimbali na kuwazawadia kutokana na kazi nzuri ya kuuza na kuutangaza utalii wa Tanzania, katikati ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Meena.
 
Bw. Hans Warburg Mkurugenzi wa Masoko wa Pongo Safari & Tours akipiga picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki mara baada ya kampuni yao kujinyakulia tuzo hiyo.
Mwanahabari Angela Msangi kutoka Shirika la Utangazaji la Taifa TBC akiwajibika vilivyo katika maonyesho ya WTM nchini Uingereza kama anavyoonekana katika picha akiwa ameshika video Camera akiendelea na majukumu yake..
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika dhifa hiyo kabla ya kukabidhi tuzo kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika kuuza na kutangaza utalii wa Tanzania, wa pili kutoka kulia ni Balozi Peter Kallaghe watatu kutoka kulia ni Issa Ahmed Othman Mshauri wa Rais Zanzibar Masuala ya Utalii na kulia ni Bw Yusuf Kashangwa Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Mkurugenzi wa Biashara Shirika la ndege la Precision Air nchini Tanzania Bw. Patrick Ndekana akiwa na Yvonne Baldwin kutoka shirika hilo wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea katika dhifa hiyo iliyofanyika kwenye banda la Tanzania.
 
Rais wa Kampuni ya Bradford Group kutoka nchini Marekani BiKarren Hoffman ambaye ni mwakilishi wa bodi ya Utalii (TTB)nchini Marekani akiongea katika hafla hiyo , ambapo ameyapongeza mashirika mbalimbali yanayofanya kazi kwa karibu na na Bodi ya Utalii Tanzania kwa jinsi yalivyosaidia kukuza utalii wa Tanzania , katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa (TTB) Devotha Mdachi na kushoto ni Meneja Masoko wa (TTB) Bw. Geofrey Meena
 
Wageni mbalimbali wakiwa katika dhifa hiyo ilipokuwa ikiendelea kwenye banda la Tanzania.
 
Hafla hiyo ikiendelea huku washiriki mbalimbali wa maonyesho ya WTM kutoka Tanzania wakifuatilia matukio mbalimbali.

No comments:

Post a Comment