.

.

.

.

Saturday, November 24, 2012

TRL KUONGEZA MABEHEWA USAFIRI WA DSM


KAMPUNI ya Reli Tanzania(TRL) imesema abiria wanaopata huduma ya usafiri wa Treni katika Jiji la Dar es Salaam wanafikia idadi ya 5000 kwa kila siku kupitia mizunguko yote miwili.
Akijibu maswali kwa njia ya mtandao Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo, Mhandisi Kipallo Kisamfu alisema kila mzunguko mmoja treni inabeba abiria 300 kwa nauli ya mwanafunzi na mtu mzima ambapo inadaiwa idadi ya abiria inazidi kuongezeka.
“Kwa kutambua hilo Mikakati ya kuboresha huduma hii ipo na  kuanzia alhamisi ya Novemba 22, mwaka huu,TRL imeongeza mabehewa mawili zaidi na hivyo kuwa manane kutokana na ongezeko la abiria wanaosafiri kufikia  zaidi 300 kwa kila mzunguko wa safari”alisema Kisamfu.
Kisamfu aliongeza kuhusu uharibifu wa mabehewa hali hiyo ni tatizo la usafiri wowote kwa umma ambapo hata Waziri wa Uhukuzi Dk Harrison Mwakyembe aliwahi kutoa  wito akiwataka Wakazi wa jiji kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa viti na vifaa vingine katika mabehewa vitendo .
Aliongeza kuwa hata suala la usalama wa abiria ndani ya treni kila abiria anapaswa kutoa udhirikiano wa kulinda uharibifu kutokana na uhaba wa askari wanaosimamia usalama katika treni hizo.
“Wito kwa wale abiria wema wawadhibiti wenzao ambao wanawashuhudia wakitoboa viti na kuvunja vioo kwa vile kila behewa linakuwa na wastani wa abiria 150 ni vigumu askari mmoja kuwaona hao abiria watukutu kirahisi bila ya 'kuchongewa na wenzao waadilifu”alisema Kisamfu.
Akizungumzia ukarabati wa mabehewa machakavu yanayoonekana katika karakana za TRL Kisamfu alise mabehewa hayo hukarabatiwa kutokana na kiasi cha fedha zikipatikana na kurejeshwa tena katika huduma za reli.
“Kwa mfano katika mradi wa mabehewa 31 ambayo yameanza kukarabatiwa tokea mwezi Juni mwa huu, 14 kati ya hayo ni ya mradi wa treni ya jiji na 17 ni kwa ajili ya treni kutoka  Dar kwenda  Mwanza”alisema Kisamfu.
Kuhusu usumbufu unaojitokeza kupitia malipo ya chenji Kisamfu alisema TRL kwa sasa inajadiliana na Kampuni ya Selcom Wireless kuboresha  huduma ambapo muda sio mrefu kutawepo utaratibu mpya wa kununua tiketi kwa wingi ambazo abiria ataweza kuzitumia kwa muda mrefu.
“Endapo Abiria atakutwa na tiketi haina alama ya mashine atahesabika kuwa amepanda bure na kustahili adhabu kwa mujibu wa taratibu,Hata hivyo kwa sasa Wakaguzi wanaendelea kukagua tiketi zetu na tahadhari tunayoitoa kwa wateja kuwa tiketi za huduma hii zinazotumika ni zile zenye tarehe ya siku husika ”alisema Kisamfu.

No comments:

Post a Comment