.

.

.

.

Friday, March 29, 2013

WENGI WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA YA GOROFA KUPOROMOKA JIJINI DAR ES SALAAM



 Jengo la Ghorofa 14 lililokuwa likiendelea kujengwa pembeni kabisa mwa Msikiti wa SHIA Mtaa wa INDRA GHAND na Zanaki, limeporomoka na kusambaratika na kusababisha vifo vya watu kadhaa ambao hadi sasa idadi haijaweza kupatikana kutokana na waokoaji kukosa vifaa vya kutosha katika zoezi hilo la uokoaji. Imeelezwa kuwa ghorofa hilo limeporomoka leo asubuhi majira ya saa moja na nusu ambapo ulianza kusikika mlio kama 'Tetemeko la ardhi'. 
Aidha imeelezwa kuwa katika Jengo hilo walikuwepo mafundi ambao walikuwa wakiendelea na ujenzi na chini alikuwepo Mama Lishe, aliyekuwa akiuza chai na eneo hilo pia walikuwapo watoto wadogo ambao haikuweza kufahamika idadi yao waliokuwa wakicheza eneo hilo, ambao wote inasemekana wamefukiwa na kifusi cha ghorofa hilo, huku waokoaji wakifanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye hata hivyo imeelezwa hali yake ilikuwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali.
 Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
 Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
 Watanzania waliokuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
 Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
 Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.
 Waokoaji wakiwa hoi......
 Juhudi zinaelekea kulala.........
 Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
 Trekta likiendelea kuondosha kifusi......../
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akihojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo.
 Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka.


PICHA KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO

1 comment:

  1. WA BONGO KILA KITU CHAO CHA UONGO MARA GOROFA 10.11,16,15
    SASA TUELEWE VIPI UONGO MPAKA KWENYE VITU VINAVYOONEKANA

    ReplyDelete