.

.

.

.

Tuesday, May 28, 2013

JAMBO CONCEPTS YAANZA MATANGAZO YA ELECTRONICS KWENYE VIWANJA VYA NDEGE DAR ES SALAAM


Pichani Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Juma Pinto akiwa na Mkurugenzi wa masoko,Mabakila na mafundi waliotoka Dubai kufunga Csreen hizo uwanja wa ndege wa JNIA juzi tayari kwa kuanzia kazi.
Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited, sasa imeingia kwenye biashara ya kisasa zaidi ya matangazo kwa kuweka electronic billboard kwenye viwanja vya ndege Tanzania.Kwa kuanzia imeanza na kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere kwa kuweka LCD screen kubwa ya 9 X 3 na inapeleka kwenye viwanja vya ndege vya KIA na Mwanza.Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo,Juma Mabakila alisema lengo kubwa ya kuweka LCD Screen kuba kwa viwanja vya ndege vya Tanzania ni kuondokana na viwanja vyetu kuweka matangazo ya kisasa ili kwenda na wakati na hususani kuweka matangazo sehemu yote ili kuondokana na utaratibu wa sasa ambao unaonekana kama hauna mpangilio.
Mbali na kuweka Screen hizo viwanja vya ndege pia itaanza kuweka katikati ya miji mikubwa ya Tanzania, kwani mbali ya kuweka matangazo lakini itakuwa kivutio na kupendezesha miji, tayari kwa kuanzia ipo mbioni kuanza na Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.

No comments:

Post a Comment