.

.

.

.

Friday, May 31, 2013

MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA MSANII NGWAIR


Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya Maziko.
Mpaka sasa ushirikiano tulioupata ni kampuni ya Clouds Media Group ambayo imebeba jukumu la kusafirisha mwili wa marehemu kutoka South Africa mpaka Tanzani, Bongo Records wameshachangia shilling milion 5 na Push Mobile wametoa million 5. Kamati inaomba wizara husika, mashirika, makampuni pamoja na watu binafsi kutoa michango yao katika kukamilisha jukumu la kumhifadhi katika nyumb yake ya milele ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha.
Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:
Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738
Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB

No comments:

Post a Comment