.

.

.

.

Sunday, August 18, 2013

DORICE MOLLEL NDIYE REDDS MISS ILALA 2013
Miss Tabata  Dorice Mollel  (22) usiku wa ijumaa aliwashinda warembo wengine 13 kushinda Redds Miss Ilala 2013 katika shindano iliyofanyika kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar es Salaam.
Dorice alimrithi Noela Michael ambaye alishinda taji hilo mwaka jana pia akitokea Tabata.
Dorice alizawadiwa 1.5milioni/-, na mshindi wa pili Alice Isaac (Dar City Centre) alipata 1milioni /-.
Mshindi wa tatu katika shindamo hilo ni Clara Bayo (Dar City Centre) ambaye  alizawadiwa 700,000/-. Mshindi wanne Pendo Lema (Tabata) alizawadiwa 400,000/- na watano  Shamim Mohamed alipata 300,000/-.
Mrembo Juanita Kabunga kutoka Tabata alizawadiwa 500,000/- baada ya kushinda Miss Talent na Kabula Kibogoti pia kutoka Tabata alishinda taji la Miss Rio and Spa na kuzawadiwa 200,000/- na ajira ya kudumu kwenye kampuni hiyo.
Warembo waliosalia kila moja alipata kifuta jasho cha 200,000/-.
Warembo hao ni Clara Paul, Anna Johnson, Irene Mwelolo, Rehema Mpanda,  Martha Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed,  Kazumbe Mussa, Kabula Kibogoti na Juanita Kabunga.                                          TATU BORA


TANO BORANo comments:

Post a Comment