.

.

.

.

Sunday, October 13, 2013

VIONGOZI WA AFRIKA WAMKINGIA KIFUA RAISI UHURU KENYATTA


Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, wamekubaliana kuwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya  hatahudhuria  kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC.
 

Katika azimio lao viongozi wa Afrika wamesema kuwa kiongozi yeyote wa taifa hatatakiwa  kuhudhuria mahakama yoyote ya kimataifa wakati yuko madarakani.

Viongozi  hao  wamefikia  maazimio  hayo  baada  ya  kuishutumu   ICC kuwa na kigeugeu – kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.

Mkutano huo  umekusudia kuwatuma Marais watano wa Afrika nchini Uholanzi ili kuitaka Mahakama hiyo kuahirisha kesi ya rais Kenyatta itakayoanza November 12 ambapo pia mkutano huu umesema hata Naibu Rais William Ruto hafai kushtakiwa kwenye Mahakama hiyo ya ICC.

1 comment: