.

.

.

.

Friday, March 07, 2014

KIZAZAA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Halima Mdee, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), akiwa haamini kinachoendelea kwenye ukumbi wa bunge wakati wajumbe wa bunge hilo walipocharuka jana na hivyo kumlazimisha mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Pandu Ameir Kificho, kuliahirisha kwa muda ili kuepusha uchafuzi zaidi wa "Hali ya Hewa"


Mbuneg MosesMachali
Christophe Ole Sendeka, naye hakuwa nyuma kwenye "sheshelumbe" la Jana Alhamisi Machi 6, 2014

BUNGE maalum la Katiba, Jana Alhamisi Machi 6, 2014, liligeuka uwanja wa “Mapambano” kama ile vita iliyotikisa ulimwengu, vita ya Kosovo kule eneo la Balkan.

Hata hivyo sio mapambano ya ngumi bali Majibishano makali yalizuka wakati wajumbe wakiendelea kujadili kanuni zitakazokuwa dira ya kuliongoza bunge hilo maalum, ambalo linaketi pale “mjengoni” kwenye ukumbi wa Bunge la Tanzania mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, alilazimika kuliahirisha bunge hilo kwa takriban masaa manne, baada ya sintofahamu iliyohanikiza ukumbi huo unaochukua takriban watu 700.

Malumbano hayo yalikuwa ni kati ya wajumbe na mwenyekiti wakati mwingine wajumbe kwa wajumbe, picha kadhaa zilizopigwa na waandishi wa habari wakati sakata hilo likiendelea, zinaonyesha, wajumbe kama vile, Christopher Ole Sendeka, Waziri wa sheria na katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamisi Bakari,Moses Machali na wajumbe wengine kadhaa, wakitoa maneno makali dhidi yao wao wenyewe na wakati mwingine wakimtuhumu mzee Kificho kwa upendeleo.

Baadhi ya wajumbe wa bunge hilo, kama Halima Mdee, kuna wakati alionekana akiwa ameshikwa na butwaa asiamini kinachoendelea ukumbini.

Kasheshe hizo zinajiri huku wajumbe hao wakiwa hata kuapishwa bado, na wachambuzi wa mambo wanabashiri kuwa hata mpango wa Ikulu wa kutaka hotuba ya uzinduzi wa bunge hilo kufanyika wiki hii huenda usifanikiwe kwani hata uchaguzi wa mwenyekiti bado kufanyika na kazi ya kuapisha wajumbe hao zaidi ya 600 huenda ikachukua hadi siku tatu.

Hebu muone uyu naye.....
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda(Katikati) na wazito wengine, wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila baada ya kutokea kizaa zaa
Wajumbe wa bunge maalum la Katiba, wakitoka ukumbini baada ya kuahirishwa kwa muda kufuatia sintofahamu iliyotokea
Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakar

No comments:

Post a Comment