.

.

.

.

Tuesday, December 22, 2015

TAMASHA LA KRISMASS WIKI HII KUPAMBWA NA REBECCA MALOPE

MWIMBAJI nguli wamuziki wa Injili Afrika, Rebecca Malope (pichani) anatarajia kuwasili nchini Desemba 24 tayari
kuja kuungana na waimbaji wengine wa ndani na nje kupamba Tamasha la KRISMASS litakalofanyikaDesemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijiji Dar es Salaam.
Akithibitisha hilo jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo la kimataifa, Alex
Msama, Malope atawasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere
majira ya saa tisa alasili. 
Msama alisema
ingawa Malope atawasili kesho, wasaidizi wake watatua nchini leo kwa ajili ya
kufanya maandalizi ya awali kuelekea tamasha hilo ambalo tayari limekuwa gumzo kubwa kwa
wapendwa, wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili.
Alisema, mwimbaji
Faustine Munishi kutoka Kenya,
aliwasili tangu jana usiku akitokea huku mwimbaji Sarah K pia kutoka nchini Kenya, naye akitarajia
kuwasili kesho majira ya saa 10 jioni.
Msama mwasisi wa
matamasha ya muziki wa injili tangu mwaka 2000, alisema Solomon Mukubwa anatarajia
kutua nchini Ijumaa asubuhi na kueelekea moja kwa moja ukumbini kufikisha
ujumbe wa neno la Mungu kwa Watanzania.
Aidha, Msama ametumia
fursa hiyo kutoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ili kurudisha
shukrani kwa Mungu baada uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani.
“Nawasihi wapendwa
wa Mungu, wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili, wajitokeze kwa wingi katika
Ukumbi wa Diamond Jubilee tuburudike pamoja na kumrudishia Mungu shukrani baada
ya kuvuka salama katika Uuchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu,”
alisema Msama.
Kwa upande wa viingilio
katika tamasha hilo, ni shilingi 50,000 kwa Viti maalum, VIP shilingi 10,000,
shilingi 5000 viti vya kawaida na shilingi 2000 kwa watoto.

“Viingilio
tulivyopanga vitasaidia wenye uhitaji maalum kama
yatima, walemavu, wajane na wengineo ambao wanahitaji msaada,” alisema Msama.
Waimbaji wengine
katika tamasha hilo ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca Honore, Christopher
Mwahangila, Joshua Mlelwa, Martha Mwaipaja, Christina Shusho, Sifael Mwabuka,
Kwaya ya KKKT  Yombo na Kwaya ya
Wakorintho wapili ambayo itazindua albamu yake ya Mchepuko sio dili.
Waimbaji wa nje ni
pamoja na Rebecca Malope (Afrika Kusini), Sarah K, Solomon Mukubwa na Faustin
Munishi ‘Malebo’  (Wote kutoka Kenya).Msama alisema mgeni rasmi katika tamasha hilo
ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye

No comments:

Post a Comment