Pichani ni Morogoro jana asubuhi. Mfuko mmoja wa machungwa shilingi elfu moja. Bado ukitaka utakatiwa chungwa la kuonja uthibitishe utamu wake. Kule Matombo, Morogoro watoto wanacheza mpira kwa kutumia machungwa. Kuna wanaocheza 'mdako' pia kwa kutumia machungwa. Machungwa ni bwelele, yanaozea mitini. Hayana soko. Wakati huo huo kwenye 'shopping centres' zetu Watanzania wananunua juisi za machungwa za kwenye makopo na plastiki kutoka Afrika Kusini na hata Ulaya. Kuna wanaodai kuwa Watanzania tumerogwa ! Je, ni kweli? Na kama ni kweli, nani ni mchawi wa Watanzania?
KWA HISANI YA MJENGWA MAJJID
No comments:
Post a Comment