.

.

.

.

Monday, September 29, 2008

MR NICE KUREJEA KWENYE GAME


Baada ya kimya kirefu,msanii wa kizazi kipya maarufu kwa jina la Mr Nice anatarajia kuingiza sokoni albam yake mpya itakayoenda kwa jina la 'Wakinuna' mnamo Oct mwaka huu. Albam hiyo itakwenda kwa style ya mafumbo kama ya muasisi wa muziki wa Reggae duniani, marehemu Bob Marley. Mr Nice, aliyewahi kutamba na kujizolea umaarufu mkubwa katika nchi za Afrika Mashariki kwa style yake ya 'Takeu', amesema anakuja kitofauti katika albam hii mpya akiwa amejaza nyimbo zilizo katika mahadhi tofauti yakiwemo yale ya 'zouk' ambao umewang’arisha wasanii wengi ambao, hata hivyo, hawakuweza kudumu kwa muda mrefu.Nice, ambaye jina lake halisi ni Lucas Mkenda, alitamba na albamu yake ya kwanza iliyoitwa 'Kidali Po', ambayo iliuzika ile kinomasana katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.Albamu lake la pili ya 'Sasambua' halikuweza kubamba na hivyo kujikuta akipotea machoni mwa wapenzi wasiotabirika wa muziki wa kizazi kipya.

No comments:

Post a Comment