.

.

.

.

Tuesday, October 14, 2008

BABU SEYA KUTUMBUIZA GEREZANI LEO

Mwanamuziki Nguza Viking 'Babu Seya' na wanae, ambao wanatumikia kifungo cha maisha katika gereza la Ukonga Dar, leo jumanne watapiga muziki wa bendi kwa ajili ya kuwaburudisha wafungwa wenzao katika Bonanza la Wafungwa lilioandalia na Global Publishers kupitia gazeti lake la Championi. Hayo yamethibitishwa na kamishna Mkuu wa Magereza nchini Tanzania, Augustino Nanyaro mbele ya waandishi wa habari katika Makao Makuu ya jeshi hilo yaliyopo Mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar. Bonanza hilo limeandaliwa maalum katika kusherehekea Nyerere Day na ni la kwanza kufanyika nchini.

No comments:

Post a Comment