.

.

.

.

Sunday, October 19, 2008

MAAJABU YA PETE BONGO

Omari Hamisi ,28, yule jamaa aliyekumbwa na balaa la pete kung`ang`ania vidoleni, kisa chake kinaendelea kuleta msisimko mkubwa baada ya yeye mwenyewe kueleza bayana kwamba tangu avae mipete hiyo, hana amani kabisa. Akiongea na gazeti hili, Omari amesema usiku anapokuwa usingizini hupatwa na hali isiyo ya kawaida. Anasema hali hiyo ya ajabu haikuwahi kumpata kabla ya kuokota pete hizo na kuziweka vidoleni mwake. Amesema hali hiyo imekuwa ikimtokea kwa miaka mitatu sasa tangu alipovaa pete hizo. ``Tangu nizivae miaka mitatu iliyopita, sikuwahi kuzivua usiku huwa napatwa na hali nisiyoielewa ambayo kabla ya kuzipata sikuwa nayo,`` anadai. Wakati Omar mwenyewe anaeleza hayo, Mtabiri maarufu katika nchi za Afika Mashariki, Sheikh Yahaya Hussein amejitokeza na kutoa maelezo aliyodai kuwa yataokoa maisha ya kijana huyo. Kijana huyo aitwaye Omari Hamisi , 28, ambaye hadi sasa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa, MOI na madaktari wanahaha kutafuta namna ya kumsaidia. Akizungumza leo, Sheikh Yahaya amesema kama kitendo cha pete hizo kung`ang`ania vidoleni kinahusiana na mambo ya kishirikiana, basi kinachotakiwa kufanywa ni kumenya vitunguu swaumu, kuviponda ponda na kisha kufukiza huku moshi wake ukielekea kwenye vidole hivyo. Amesema iwapo pete hizo ni za majini basi yatatimuka, na madaktari wataweza kufanikiwa kuzitoa kwa kuzikata bila matatizo. ``Kuna majini huwa yanatupa pete na mtu anapookota basi anaweza kupata matatizo kama hayo,`` amesema. Ameongeza kuwa iwapo zoezi hilo la kitunguu swaumu halitafanikiwa, basi ni budi zitafutwe njia nyingine za kumsaidia kijana huyo. ``Siku ya kwanza tulianza kazi ya kuondoa pete zile kwa kutumia sabuni na mafuta, lakini ilishindikana baada ya kuonekana kuwa ngumu kiasi cha kutisha,`` alisema mmoja wa wauguzi ambaye hakutaka jina lake litajwe. Hata hivyo, madaktari hawakuishia hapo kwani waliamuru apelekwe katika chumba maalum chenye vifaa vya kuondolea vyuma mwilini, huko ndipo maajabu ya pete hizo yalipoanza kuonekana. Inasemekana kila walipozigusa kwa mashine hiyo kwa nia ya kuzikata, zilitoa cheche za moto ambao ulikuwa ukimuunguza mgonjwa huyo. Hata hivyo, alipoulizwa Afisa Uhusiano wa MOI, juu ya sakata hilo, alisema mgonjwa huyo bado anaendelea kulazwa hospitalini hapo wakati madaktari wanaendelea kufikiria njia ya kuondoa pete hizo ambazo zimesababisha vidole vyake kuanza kuvimba.

No comments:

Post a Comment