.

.

.

.

Tuesday, October 14, 2008

MAGARI YATOKOMEA USIKU

MSHINDI WA JIMBO LA TARIME MH.CHARLES MWERA


VIONGOZI wa juu wa CCM pamoja na wafanyabiashara ambao magari yao ya kifahari (mashangingi) yalikuwa yakirandaranda wilayani Tarime wakati wote wa kampeni za uchaguzi wa ubunge na udiwani, juzi yalitoweka usiku wa manane baada ya kupata uhakika kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimezoa viti vyote viwili.
Chadema ilifanikiwa kurejesha viti vyake viwili vilivyotangazwa kuwa wazi baada ya kifo cha Chacha Wangwe, aliyefariki kwa ajali ya gari zaidi ya miezi miwili iliyopita baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya vyama vingine vitatu, kikiwemo chama tawala cha CCM.
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Tarime, Triasis Kagenzi alimtangaza mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, Charles Mwera Nyanguru kuwa mshindi baada ya kuzoa kura 34,545 na hivyo kumwacha mbali mgombea wa CCM, Christopher Ryoba Kangayo, aliyepata kura 28,996.

No comments:

Post a Comment