.

.

.

.

Monday, October 13, 2008

ORiGINAL COMEDY (ZE COMEDY)

Kundi la vichekesho la Origino Komedi linatarajia kufanya onyesho la kwanza la wazi siku ya familia iliyoandaliwa na Kampuni ya OZ Media Limited itakayofanyika Oktoba 18 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Onyesho hilo litakuwa la kwanza tangu kundi hilo lilipobadili jina kutoka lile la mwanzo lililojulikana kama ‘The Comedy’.Kubadilika kwa jina kutoka The Comedy na kuwa Origino Comedy kulitokana na mgogoro wa haki miliki uliyokuwepo kati ya kundi hilo na kituo cha Televisheni cha East Africa na kupelekea Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) na kuingilia kati na baadaye suala hilo kufika katika mahakama ya Biashara.Akizungumza jijini Da es Salaam jana, Mratibu wa shoo hiyo, Ruhembe Mwamba alisema kuwa mbali na Origino Komedi pia Bendi ya Vibration Sound itatoa burudani.

1 comment:

  1. Nawapenda sana, hako kashotiii mbona mmekafunika jamani?

    ReplyDelete