.

.

.

.

Monday, October 20, 2008

YANGA YAZIDI KUPAA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Bara, Yanga, jana walizidi kujichimbia kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 24 baada ya kuifunga Polisi Dodoma katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pointi hizo, zinatokana na mabingwa hao mara 21 wa ligi hiyo tangu mwaka 1965, kushinda mechi nane kati ya tisa ilizocheza tangu kuanza kwa Ligi hiyo Agosti 22.
Aidha, ushindi huo umeiweka Yanga katika nafasi nzuri kisaikolojia kwani ni siku sita tu kabla ya kukutana na mtani wake wa jadi Simba, ambaye juzi alitandikwa mabao 4-1 na Toto African ya Mwanza.
Hivyo, wakati Yanga ikipoteza mechi moja, Simba inakutana na Yanga, ikiwa imepoteza mechi nne, hivyo kuwa na pointi 13, ambazo ni pungufu kwa pointi 11.

No comments:

Post a Comment