.
.
Friday, November 21, 2008
KOMBE LA CHALENJI 08/09
TIMU ya Tanzania imepangwa kundi moja na wenyeji Uganda na Rwanda kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yaliyopangwa kuanza rasmi Desemba 31 hadi Januari 15 nchini Uganda.
Tanzania ipo kundi A na ndugu zao wa Zanzibar, Rwanda, Somalia na wenyeji Uganda. Katika mechi ya ufunguzi Zanzibar watakata utepe kwa kumenyana na Somalia kabla ya Uganda kuwakaribisha Rwanda.
Kundi hilo la A linaonekana kuwa na pinzani mkali kutokana na timu zilikuwemo humo Rwanda na Uganda kuwa na upinzani mkali wakati Somalia na Zanzibar zikitabiriwa kuwa vibonde wa kundi hilo kutokana na mara kadhaa kutoonyesha upinzani katika mashindano yanayoandaliwa na Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo kutakuwa na timu ya Saud Arabia na Zambia ambayo ilishaalikwa katika mashindano hayo mwaka juzi yalipofanyika Ethiopia na ilifanikiwa kutwaa ubingwa ikiwa chini ya Patrick Phiri na kukabidhiwa kitita cha dola 30,000 bila kikombe.
Kundi B lina timu za Sudan, Kenya, Burundi na vibonde Elitrea na Djibout timu hizo zitakuwa kwenye uwanja wa Jinja huku Ethiopia ikikosa mashindano hayo kutokana na kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa na Shirikisho la Soka duniani (FIFA), kutokana na migogoro iliyogubika ndani ya shirikisho hilo la Ethiopia.
Tayari Shirikisho la Soka Tanzania limeweka wazi mikakati ya timu ya taifa Taifa Stars kuwa kambi ya timu hiyo haitavunjwa na badala yake wachezaji wataendelea kuwa kambini mpaka Desemba 14.
"Desemba 14 hadi 27 wachezaji watapumzika na hapo katikati kuna mashindano ya kombe la Tusker, itarudi tena kambini Desemba 28 kwa siku mbili kujiandaa na Chalenji,"alisema Mwakalebela.
Michuano hiyo ya Chalenji itaonyeshwa live na kituo cha televisheni cya Gate way 'GTV' ambacho kimedhamini mashindano hayo kwa dola 500,000.
Jumla ya zawadi zitakazotolewa ni shilingi dola 60,000 mshindi wa kwanza akipata dola 30,000 mshindi wa pili dola 20,000 wakati mshindi wa tatu atajipatia dola 10,000.
Michuano hiyo inashirikisha nchi za Kenya, Zanzibar, Rwanda, Burundi, Tanzania, Eritrea, Djibout, Somalia Uganda na Sudan ambaye ndiye bingwa mtetezi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment