.

.

.

.

Monday, December 29, 2008

NDOA ZA MASTAA WA BONGO

Ukweli umedhihirika kuwa, mpaka mwaka huu unaingia kaburini, ndoa 6 za mastaa zimevunjikia kwa mbali na kuwaacha ‘wahanga’ wakiwa hawaamini kilichotokea.Ndoa zilizodhihirika kusambaratika ni pamoja na mwanamuziki maarufu nchini na kiongozi wa Bendi ya T-Respect, Ali Choki Luambo.Ndoa nyingine ni ya mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds FM, Violet Chrisant Mzindakaya ‘Sista V’ na kada na wa CCM, Mr Mpogole.Kama vile risti ni ndogo, ikajagundulika kuwa, ndoa ya msanii wa Filamu nchini, Mohamed Mwikonge ‘Frank’ nayo iko miguu juu kichwa chini kisa kikisemekana ni nyota huyo kupata kipya kinyemi chenye ‘figa’ iliyokwenda shule.Treni hilo la wenye ndoa zilizovunjika halikumwacha mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Mohamed Mpakanjia ‘Meddy’ ambaye juzi kati amekiri kumpiga chini mwanamke aliyemuoa mwaka juzi, Aisha Bui, mkazi wa Kigamboni, jijini Dar.Katika utetezi wake mbele ya waandishi wetu, Meddy alidai kisa cha kumpiga chini Aisha ni tabia mbaya, hakuna kingine.Wakati Aisha anashikilia talaka yake mkononi, Dida naye, amejikuta akitemana na mumewe ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Mchopange ‘Mr Mchops’ kisa kikisemekena kuwa ni tabia chafu ya mmoja wa wana ndoa hao.Hivi karibuni, Bosi wa mashindano ya Miss Tanzania, Anko Hashim Lundenga naye amejikuta akipanda kizimbani, mkewe, mama nanihii, akimtaka ampe talaka yake na kumgawia sehemu ya ‘utajiri’ waliovuna wote, kwani ndoa yao imeota mbawa.Lundenga anasemekana kuoa kimwana mmoja ambaye amewahi kuwa Miss Tanga. Yeye mwenyewe alipoulizwa alikiri yote hayo, kuoa, kutengana na mkewe na kufikishwa mbele ya Pilato. Hata hivyo, wakati mastaa hao wakilia chini kwa chini kwa ndoa zao kuvunjika na pengine wakiwa hawataki tena kusikia habari za ndoa, wenzao wamezikimbilia na kuzifunga.Ndoa zilizofungwa, hasa mwaka huu wa 2008 ni pamoja na Miss Tanzania, 2004, Faraja Kota ambaye amechukuliwa jumla na Mbunge wa Chama Tawala (CCM) mkoani Singida.Baada ya hapo, akafuatia msanii na mfanyabiashara wa jijini Dar, Husna Shaban ‘Dotnata’ ambaye amejifunga kwa mwanajeshi mstaafu, Mohamed Poshi.Mbali na Dotnata, aliyekuwa nyanda nambari wani wa timu ya Simba, Juma Kaseja ambaye kwa sasa anazuia michomo isiingie kwenye goli la Yanga naye ameutumia mwaka huu, 2008 kufunga ndoa na Nasra Nassoro.Mr Dar, 2005 Mwinyi Ahamed, ambaye bado ana harufu ya skendo ya kumwingiza ‘town’ Miss Tanzania 2008, Nasreen Karim, yeye aliingia kwenye mnyonyoro huo, mwezi wa saba mwaka huu na mpenzi wake, Witney Sylvester ambaye kwa sasa anaitwa Zahra. Nyota mwingine ambaye ameungana na wenzake kuoa ni m-Bongo Fleva, Z. Anto, yeye ameopoa kimwana na kukimiliki miezi si mingi.Baada ya kufanya tukio hilo ambalo lina baraka za Mungu, mwanamuziki mwingine wa Bongo Fleva, Y-Dash naye alijitutumua na kuamua kuvuta ndani kwa ndoa halali kabisa.Kuona hivyo, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’ naye akasogeza ndani mwake, katika ndoa iliyofungwa kanisa la Azania Front na sherehe zake kufanyika Ukumbi wa Princess uliopo Sinza Mapambano.Mwingine aliyeamua kuutumia mwaka 2008 kuuaga ukapera ni Seif Shaban ‘Matonya’ ambaye alifunga ndoa na mwanamke aliyejulikana kwa jina moja tu la Mariam.Msanii wa runinga nchini, Christine John Manongi anaweza kuwa ndiye aliyefunga mwaka huu kwa kuolewa. Ndoa ya msanii huyo imefanyika siku chache zilizopita jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu kibao.

Katika yote, kubwa ambalo linaonekana kuwashangaza wengi ni kitendo cha nyota wawili kuachana na ndoa kisha kuoa au kuolewa.Nyota hao ni Dida ambaye mwaka huu huu amefunga ndoa nyingine huku ile ya kwanza ikiwa bado inamalizikia kukata roho.Mohamed Mwikonge ‘Frank’ naye baada ya kumkimbiza nje ya nyumba mkewe wa kwanza, mwaka huu
SoUrCe: IJUMAA WIKIENDA

No comments:

Post a Comment