
wadau hao walisema kuwa tatizo kubwa lililommaliza mrembo huyo ni saikolojia.Wakichambua pointi hiyo, wadau hao walisema kuwa kitendo cha mlimbwende huyo kushinda taji la Miss Tanzania Agosti 2, mwaka huu kisha fainali za dunia kufanyika Desemba 13 ni kipindi kifupi ambacho hakitosholezi kumuandaa mrembo.Walitolea mfano baadhi ya warembo wa nchi nyingine ambao walipatikana mwaka mmoja kabla, hivyo kupigwa msasa na kuandaliwa vizuri kisaikolojia kwa ajili ya shindao.
Pointi nyingine iliyoelezwa kuwa sababu ya Nasreen kuchemka ni skandali la kutembea na mume wa mtu, Mwinyi Ahmed ambalo liliibuliwa na gazeti hili kabla ya kupokezana na ndugu yake, Ijumaa na kuvuma kwa zaidi ya mwezi mzima.“Unajua ile skendo itakuwa ilimchanganya sana, ukizingatia liliibuliwa na kuvuma siku chache kabla hajakwea pipa kuelekea Afrika Kusini,” alisema Idrisa Kibene wa Sinza, Dar es Salaam.
Sababu nyingine iliyoelezwa ni mazingira ya nchini Afrika Kusini kwa sababu Nasreen alikuwa hajaizoea nchi hiyo, mpaka pale alipokwenda mwezi mmoja uliopita.Katika pointi hiyo, Miss Tanzania 1999-2000, Hoyce Temu, alisema juzi kupitia TBC1 kuwa: “Nasreen hajapata muda wa kutosha, mimi nilifuatilia haya mashindano, nikamsoma Miss India mwaka huu ndani ya kipindi kifupi ametembelea Afrika Kusini mara tatu kabla ya mashindano.
Mrembo aliyeibuka mshindi ni Miss Urusi, Kseniya Sukhinova, wa pili Gablielle Walcott wa Trinidad na Tobago, wakati mrembo wa India, Parvathy Omanakuttan aliibuka namba tatu.Warembo wengine waliobahatika kuingia tano bora ni Brigite Santos wa Angola na Tansey Coetzee wa Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment