.

.

.

.

Monday, January 05, 2009

AJALI MBAYA MOSHI YAUA 10

WATU 10 wamefariki dunia papo hapo na wengine kumi kujeruhiwa vibaya, baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kuligonga kwa nyuma lori la mizigo katika eneo la Mabungo barabara kuu ya Moshi- Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko amesema kwa simu jana kuwa, ingawa yuko nje ya mkoa wa Kilimanjaro, lakini amejulishwa kuhusu ajali hiyo mbaya iliyotokea saa mbili kamili usiku.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali watu nane walifariki dunia papo hapo na wengine wawili walifariki dunia njiani wakati wanakimbizwa hospitali ya KCMC.
Habari zilisema kuwa basi hilo dogo lilikuwa likitokea Marangu-Moshi Vijini kuja mjini Moshi na lori lilikuwa likija mjini Moshi na inaelezwa kwamba, dereva wa basi dogo alishindwa kulimudu basi hilo na kuligonga kwa nyuma lori hilo.

No comments:

Post a Comment