.
.
Monday, January 05, 2009
BINTI WA RAIS KIKWETE ACHEZWA NGOMA
Katika hali ambayo si ya kushangaza, Rais JK amemcheza ngoma bintiye (yaani kufundwa jinsi ya kuishi na mume). Ngoma hiyo ambayo ilihitimishwa mjini Bagamoyo (viwanja vya nyumbani kwao) siku ya Jumapili tarehe 4 Januari. Sherehe hizo ambazo zilichukua takribani si chini ya siku kumi, ambapo watu walikula na kunywa zilikuwa na mabinti wawili (waliochezwa), mmoja ni mtoto wa JK na wa pili ni mtoto wa shoga yake Salma kutoka kusini ambaye alipendelea wacheze ngoma pamoja. Kwa hiyo watu walishuhudia ngoma za kimakonde, kikwere na kizaramo kwa pamoja. Aidha, bendi ya muziki ya mjini hapo, Bwagamoyo Sound ya Mwinjuma Muumini ilitumbuiza siku zote hizo za sherehe (nje) bure. Huku Salma na kundi lake wakimwaga radhi mjini hapo, JK mwenyewe aliwasili tarehe 3 Januari Jumamosi jioni (saa 1 jioni) kwa ajili ya mkesha wa kuamkia Jumapili. Eneo la sherehe lilipambwa na majukwaa ya maturubai yaliyo nakshiwa kwa unadhifu. Maturubai hayo yapatayo kama 20 yalileta maandhari nzuri hasa usiku ambapo taa za kila rangi zilizungushwa kuunganisha maturubai hayo. Ulinzi mkali ulikuwepo watu wakishuhudia wingi wa FFU na magari maalum ya Ikulu yakiwa yamepaki pembeni. Sherehe ilifana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment