.

.

.

.

Wednesday, January 07, 2009

BOSI WA UWT KUPATIKANA DODOMA LEO

Leo ni leo katika kinyang`anyiro cha uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambapo wanachama wanapiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Taifa wa umoja huo. Wagombea na wapambe wa wanaowania nafasi hiyo, wamekuwa wakipigana vikumbo kuomba kura kwa wajumbe.

Hata hiyo, kama ilivyokuwa kwa kampeni za uchaguzi wa Umoja wa Vijana, pia kumekuwa na mvutano kwa wagombea wawili ambao ni Sophia Simba na Janeth Kahama. Wapambe hao ndio wameonekana wakirushiana maneno ya hapa na pale na wengine kutoleana misemo ya kwa kutumia nyimbo za taarabu.

Mgombea mwingine ni Joyce Masunga.
Misemo hiyo ni pamoja na ``Watatuweza wapi sisi watoto wa mjini, hawana nyimbo na wameishiwa.`` Katika viwanja vya makao makuu ya chama hicho jana, wasanii walionekana wakiimba na kuwahamasisha wajumbe wamchague mmoja wa wagombea.
Aidha, imedaiwa kuwa, wapambe wa mgombea mmoja waliwaandalia chakula cha jioni baadhi ya wajumbe katika moja ya hoteli kubwa ya mjini hapa.

No comments:

Post a Comment