.
.
Sunday, January 04, 2009
KILIMANJARO STARS YAANZA VIBAYA
Timu ya taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars jana Jumamosi ilianza vibaya michuano ya Kombe la Chalenji la Afrika Mashariki na Kati, baada ya kufungwa na Somalia bao 1-0 kwenye Uwanja wa Nakivubo mjini hapa. Haikuwa siku ya furaha kwa Tanzania baada ya Zanzibar ambayo ina wachezaji wengi wa timu ya vijana nayo kulazimika kutoka suluhu na wenyeji Uganda katika mechi nyingine ya Kundi A. Bara na Zanzibar zinapambana kesho Jumatatu katika mechi nyingine ya timu za nyumbani ambayo ni lazima Stars ishinde ili kuendelea kuwa juu ya Rwanda katika msimamo. Kutokana na matokeo hayo Uganda imeendelea kuongoza Kundi A kwa uwiano wa mabao ikiwa na pointi nne, sawa na Zanzibar ambayo iliifunga Somalia 2-0 Januari mosi. Stars ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri na ilikuwa ikitajwa zaidi hapa Kampala kutokana na kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment