.

.

.

.

Tuesday, January 06, 2009

MAHAKAMA INASHUGHULIKIA OMBI LA BASIL MRAMBA

Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Da es Salaam, imesema kuwa inaendelea kushughulikia ombi la aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Pesambili Mramba la kusafiri nje ya mkoa wa Dar.Hakimu anayesikiliza kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kulisababishia Taifa hasara ya zaidi ya Sh.Bilioni 11 inayowakabili Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona, pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wizara hiyo Grey Mgonja, Hezron Mwankenja, amesema hii leo kuwa suala hilo huenda likafafanuliwa vizuri Januari 7. Mramba aliiomba mahakama hiyo hivi karibuni ili iweze kumpa kibari cha kwenda kuwasalimia wapiga kura wake.

No comments:

Post a Comment